google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 24, 2018

Kwa Nini Hutakiwi Kuonyesha Udhaifu Wako Kwa Wengine?

No comments :
Kila mmoja wetu ana udhaifu wa aina fulani. Kwa mfano, kuna wengine wana hasira, kuna wengine wana huruma, na kuna wengine hawawezi kuficha siri. Kila mmoja ukiangalia ana udhaifu wa aina fulani, hata wewe upo udhaifu ambao unao.
Pamoja na kila mtu ana udhaiafu wake, lakini kitaalamu unashauriwa usijaribu kuuweka udhaifu wako huo kwa watu wengine kwa sababu, ipo siku watu hao watakaojua udhaifu wako watautumia udhaifu huo huo kuumiza wewe.
Hata ikitokea mtu huyu ni wa karibu sana, usimwambie udhaifu wako wewe kaa nao. Ndio maana hata kwenye biashara wengine wanashinda na kufanikiwa kwa sababu ya kujua udhaifu wa upande wa pili uko wapi na kuufanyia kazi.
Si kwenye biashara tu, hata kwenye vita, au kwenye mpira, wale wanaojua udhaifu wa wengine vizuri hao ndio wanaoshinda. Kwa hiyo kuweka udhaifu wako nje ni sawa na kuanza kujitangazia kwamba ni lazima utashindwa katika eneo fulani la maisha yako.



Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.

Katika mfano huo, ingawa wengi tunajua lakini unaonyesha Samsoni siri ya nguvu zake nyingi ambazo alitumia kuulia Simba na kupiga maadui zake zilikuwa kwenye nywele. Alikuwa hatakiwi kukata nywele kwa namna yoyote ile na hiyo ilikuwa ni siri kwake ambayo hakutakiwa kusema kwa mtu.
Lakini alipoulizwa na kubembelezwa sana ataje siri ya nguvu zake na mkewe, mwisho akajikuta akiisema, aliamua kuweka udhaifu wake nje, na matokeo yake wakati amelala aliweza kukatwa nywele na kukosa nguvu hizo alizokuwa nazo na matokeo mabaya yalimkuta kwa sababu ya kuonyesha udhaifu wake nje.
Unatakiwa kujua ni kitu kibaya na hatari kwako ni kujaribu kuuweka udhaifu wako nje na kila mtu auone. Huko ni kujitakia hatari kubwa sana ambayo inaweza kukupoteza wewe. Kama una udhaifu wa aina fulani kaa kimya, sio lazima useme.
Kikubwa kwako na kitu cha kufanya ni kuufanyia kazi udhaifu wako na kuhakikisha unakuwa bora. Lakini usijaribu kuweka udhaifu wako nje hata kwa rafiki, watoto au mtu wa karibu unayemwamini kama mkeo. Ni kosa kubwa kama kweli ukiamua kuanika udhaifu wako.

Amini usiamini ipo siku utaumizwa tu kwa wewe kuuweka udhaifu wako nje kama utafanya hivyo. Kwa hiyo dawa pekee ya kuweza kukwepa kuumizwa huko ni kukaa kimya na udhaifu wako na si kusema kwa kila mtu.
Achana na tabia ile ya watu utakuta anasema aah, mimi nina hasira ujue. Watu ipo siku watatumia hasira hizo hizo kukufanyia kitu ambacho wewe hujaamini. Kitu cha msingi hapa ni kuhakikisha unafunga mdomo wako na kuweka moyoni mwako udhaifu wako.
Neno la mwisho kwangu nikukumbushe, usijaribu hata siku moja kuonyesha udhaifu wako kwa wengine, watu hao watatumia udhaifu huo kama fursa ya kuweza kukuumiza wewe. Tafakari hili na utagundua ukweli hasa wa hiki nikisemacho.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.