Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, April 21, 2016

Kinachokufanya Ushindwe Kufikia Uhuru Wa Kipesa Ni Hiki Hapa.

No comments :
Kwa wale wafatiliaji wazuri wa mtandao wetu wa dira ya mafanikio wiki iliyopita katika moja ya makala zetu tuliongelea juu ya tabia ambazo zinaweza zikakuzuia kupata kiasi kikubwa cha pesa unachokitaka. Kwa kifupi tuliona mchango wa tabia hizo katika suala zima la kukuzuia wewe kupata pesa za kutosha. Leo katika makala haya, mbali na tabia hizo tutaangalia kitu kingine cha kipekee ambacho kina uwezo mkubwa wa kukufaya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa hata kama unaweka juhudi nyingi.
Najua unatamani kujua kitu hiki ambacho kinauwezo mkubwa wa kukuzuia kupata pesa. kama ni hivyo tulia, acha kuwa na haraka sana. Kumbuka kwamba wakati mwingine, linapokuja suala la kukosa kile kiwango cha pesa unachotaka tatizo huwa sio ukosefu wa pesa, au pesa hazitoshi kama wengi wanavyodai. Tatizo huwa ni moja tu ambalo ni hofu ya kupata kiwango kile cha pesa unachokihitaji. Usishangae sana hili ndilo tatizo lingine linalokufanya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa unaoutaka.

Naona hunielewi elewi vizuri na unajiuliza maswali mengi kwamba ninaongea kitu gani? Sikiliza. Kama wewe ni mfanyakazi na unataka kujiajiri na umeona biashara fulani ndiyo itakayokulipa moja kati ya maswali ambayo utakuwa unawauliza sana watu ambao walishafanya hiyo bishara hiyo ni kwamba hivi nitapata kiasi hiki cha pesa kwa mwezi. Unajua ni kiasi gani ambacho utakuwa unauliza? Ni ile pesa ambayo unataka kujua kama itakuwa sawa na ile unayolipwa. Utakuwa una lengo la kulinganisha mshahara na pesa unayoipata kwenye biashara.
Sasa unapoona hivyo ujue hiyo ni moja ya hofu ambayo inaweza kukuzuia kufikia kwenye uhuru wa kipesa. Unapochagua kufanya biashara fanya biashara kwa nguvu zote. Kwa kadri unavyozidi kuendelea inakuwa inazidi kukua polepole na kuwa biashara kubwa kuliko ulivyokuwa ukifikiri. Lakini suala la kujijengea hofu sana litakuzuia kufikia uhuru wa kipesa usipokuwa makini. Waangalie wote wenye hofu kama waapesa. Naamini unajua hwana pesa nalo. Hofu haina msaada wowote katika maisha yako, hata wewe kama hofu yako ni kubwa huwezi kufikia uhuru wa kipesa na huwezi pata pesa pia.
Ili uweze kufikia uhuru wa kipesa jenga imani kubwa ndani yako ya kuamini kwamba hilo kwanza linawezekana. Ukishajijengea hiyo imani anza kuchukua hatua. Kwa kuchukua hatua, hiyo itakusaidia sana kufikia mafanikio makubwa. Acha kuruhusu imani ya ‘siwezi’ ikakutawala ndani yako. Kama utakuwa na imani hii basi itakuwa ni chanzo kimojawapo kikubwa cha kukufanya ushindwe kufikia uhuru wa kifedha.
Kwa leo tuishie hapa ila kumbuka endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment