Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, April 7, 2016

Siri 10 Kwa Nini Watu Wengi Hushindwa Kutimiza Malengo Yao.

No comments :
Kila mtu ana malengo na mipango mingi ya kufanya kila siku katika maisha yake. Lakini kitu cha kujiuliza mbona mipango na malengo ya wengi huwa hayatimii kama ilivyokusudiwa? Katika makala hii ya leo ungana nami nikupe siri 10  za kwa nini wengi hushindwa kutimiza malengo yao japo wanajitahidi kila siku kufanikisha malengo hayo lakini hayatimii?

1.Kushindwa kubadili tabia katika matumizi ya pesa na muda. Watu wengi hawana nidhamu katika matumizi ya pesa na muda.

2. Kutokuwa na bajeti katika matumizi ya pesa.

3. Kutokujua tofauti kati ya mahitaji muhimu na mahitaji ya lazima. Hivyo kujikuta wanatumia pesa nyingi kataka  vitu vya muhimu na kuacha vitu vya lazima.

4. Kuwa na matumizi makubwa kuliko vipato vyao. Hali inayopelekea watu kuwa na tabia za udokozi,wizi na hatimae kuwa mafisadi.


ISHI KWA MALENGO SAHIHI, UTAFANIKIWA.
5. Kutegemea chanzo kimoja tu cha mapato. Mtu kutegemea mshahara pekee au kiduka kidogo alichofungua bila kubuni mradi mwingine hii ni hatari sana.

6. Kukosa malengo sahihi katika maisha, Utakuta mtu  hajui afanye nini na aache nini katika maisha yake anakuwa yupo yupo tu ilimradi yupo duniani.

7. Kukosa mwendelezo katika mambo yakufanya. Utakuta mtu akipata hasara anakata tamaa kabisa na kuacha kufanya au akipata faida kubwa anaridhika na kwenda kutumbua kwanza hadi pesa iishe ndipo akumbuke tena kufanya.

8. Kukosa ufuatiliaji na utekelezaji wa mipango na malengo anayojipangia. Anaishia kusema tu kwa mdomo tu nitafanya hivi na vile hadi mwaka unaisha.

9. Kukosa imani katika jambo au malengo aliyopanga. Anahofu katika kufanya jambo kwa sababu anaweza pata hasara, Anaweza kata mtaji. Atalogwa na watu watamwonaje akifanya mradi au biashara ile.

10. Kukosa taarifa sahihi kwa muda sahihi. Hapa ndipo kiini cha kukosa mafanikio kilipo. Kamwe huwezi kupata mafanikio katika jambo lolote lile mpaka upate taarifa sahihi. Huwezi kuoa au kuolewa na mtu usiyekuwa na taarifa zake sahihi, huwezi kulima zao ambalo hujui utamuuzia nani, Huwezi kujenga nyumba wakati hujaonana na fundi ujenzi akupe taarifa na vitu gani ununue,huwezi kwenda chuoni kusomea fani ambayo hujui utaajiriwa na nani, Huwezi kufanya sherehe usiyojua gharama zake utazimudu? TAARIFA TAARIFA TAARIFA.

Asante kwa kunifatilia, kumbuka kuchukua hatua.

Ni wako rafiki  katika kusaka mafanikio na kuonyesha njia za mafanikio Shariff Hamisi Kisuda maarufu mzee wa Nyundo.  


No comments :

Post a Comment