Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, April 11, 2016

Mambo Mawili (2) Yenye Kuleta Mafanikio Kwa Haraka.

No comments :
Kuna wakati ni lazima utambue baadhi ya mambo ya msingi yatakayokufanya uweze kufanikiwa katika maisha yako. Mafanikio ninayoyazungumzia ni yale ya kila shughuli ambayo unaifanya ili mradi tu iwe halali katika jamii na inatambuliwa kisheria. Leo nataka kutumbua majibu ya kimafanikio ya kibiashara, kazi, masomo na mambo mengine. usishangae wala hujakosea kusoma yapo majipu ya kimafanikio ambayo yanatukwamisha tusiweze kufanikiwa. Tafadhari shusha pumzi kisha twende sawa katika makala hii utakwenda kuelewa vizuri.
Haya ndiyo mambo ya kuyafanya ili uweze kufanikiwa;
Kujitambua.
Hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi sana. Kujitambua ndio suala ambalo watu wengi hatunalo. Tafiti zinaonesha ya kuwa mtu mzima ana miaka kumi nane, pia  watu wengi  wanaamini kuwa katika kipindi cha umri huo mtu ndio anaanza kujitambua, ila ukifuatilia kwa watu walio wengi katika umri  huo utagundua hakuna ukweli,  kama ni kweli watu waliofika umri wa miaka 18 kweli wanajitambua kwa maana ya kuanza kupata mafanikio. Mbona ndio kuna wimbi kubwa la watu wanaolalamika kuhusu maisha?
Lakini kiuhalisia umri huo kwa hapa nchini ni umri wa kuwa na meno thelethini na mbili na kuruhusiwa kwenda kununua pombe ambazo mwanzo alikuwa haruhusiwi kununua, unacheka huo ndio ukweli usiopingika. Maana  yangu ni kwamba watu wengi tunachelewa sana hasa katika swala la kujitambua. Wengi wetu tupo katika kipindi cha kuamini ya kwamba ipo siku ndio tutaanza kufanya kitu fulani. Bado tunaishi katika misingi ya kuwa tegemezi na  kuamini kuwa vijana ni taifa la kesho kitu ambacho sio kweli.

WEKA VIPAUMBELE VYA MAISHA YAKO.
Shutuka ewe mwanajamii hasa kijana huku ukujiuliza wewe ni nani? na unataka kufanya nini ili uweze kufanikiwa na sio kusubiri muda fulani ndio uanze kuyasaka mafanikio. Tuendele na ufafanuzi ukiwa ni miongoni mwa vijana wanaosema ya kuwa  huu ni muda wa kula ujana basi endelea ili uje umeze uzee vizuri. Wimbi kubwa la watu ambao wanalalamika kuhusu maisha ni vijana, lakini vijana hao hao pindi wapatapo pesa hawana nidhamu sahihi juu ya matumizi ya pesa hizo. Mfano leo hii mtu anakuwa na pesa nyingi sana baada ya siku chache utamsikia anaita pesa ni shetani kwa sababu zimeisha zote bila kufanya kitu cha maana. Nataka kukwambia ewe msomaji wa makala hii mwenye tabia kama hizi, ya kuwa pesa sio shetani ila matumizi yako ndio shetani.
Tambua ya kuwa maisha mazuri ya kesho huandaliwa na leo yako ukiendelea na tabia ya kusema bado upo upo, basi utaendelea kuwepo kama friji ambalo limetulia tu ndani. Ewe kijana mwenzangu kwa kuwa unahitji mafanikio ya kweli basi ni muda sahihi wa kujua wewe ni nani na ni nini? cha kufanya ili uweze kufanikiwa katika maisha yako. Pia katika safari ya mafanikio kumbuka ya kuwa njia ya mkato ndiyo njia ndefu na yenye maisha mafupi hivyo jitahidi kutafuta mafanikio yako kwa njia iliyo halali.
Weka vipaumbele.
Katika maisha ni kwamba ni lazima ujue ni vitu gani unataka kuvifanya. Weka mikakati ambayo ni kwamba haitaishia njiani, kila jambo ambalo unalolifanya hakikisha ya kwamba hukatishi safari hiyo, kuna usemi  unasema zege hailali, basi hakikisha na wewe unafanya mambo ambayo unapata matokea chanya ya jambo hilo. Kama alivyo askari akiwa vitani basi na wewe uwe hivyo hivyo kwamba hakikisha unapambana na changamoto zote ambazo zitajitokeza mbele yako.
Makala imeandikwa; Benson Chonya
Simu: 0757-909942

No comments :

Post a Comment