Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, April 12, 2016

Unaweza Kubadilisha Maisha Yako Kabisa Ukiamua Na Kufanya Hivi.

No comments :
Moja kati ya kosa kubwa ambalo watu wengi wanafanya katika maisha yao ni kule kuamini kwamba hawawezi kufanya mambo fulani na badala yake uwezo huo wamewaachia watu wengine. Kwa mfano utakuta mtu anakwambia hawezi kufanikiwa kwa viwango vya hali juu sana kwa sababu hana uwezo huo lakini ingawa kiuhalisia sio kweli.
Chochote unachokitaka katika maisha yako, unaweza kukipata ikiwa utauamini uwezo mkubwa ulio ndani yako. Una uwezo mkubwa sana ndani yako usioelezeka ambao ukiutumia unaweza kukupa chochote ukitakacho kama tu utachukua hatua. Lakini kama utaendelea kuamini huwezi kufanikiwa ni wazi kabisa hutaweza kufanikiwa. Utapata kile unachokiamini akilini mwako.
Jiulize kama kuna watu wengine wanaweza kufanikiwa kwa nini wewe ushindwe kufanikiwa? Wanaofanikiwa kumbuka ni watu wa kawaida wenye macho, miguu, nywele, akili na kila kitu sawa na wewe. Kitu ambacho pengine wamekuzidi ni maamuzi  na kiu ya kufanikiwa kwao. Kama ni hivyo fanya uamuzi sahihi wa kufanikiwa.
Kama fulani aliweza kufanikiwa na wewe unaweza pia kufanikiwa ukiamua.
Kama Oscar Pistorius mwanariadha mlemavu aliweza kufanya hivyo na kufanikiwa wewe pia unaweza kufanikiwa kwa hali yoyote uliyonayo.
Kama Ben Carson mwandishi wa vitabu aliweza kufanikiwa akitokea kwenye mazingira magumu ya kimaskini  na wewe unaweza.

TUMIA AKILI YAKO  VIZURI KUKUFANIKISHA.
Kama Aliko Dangote aliweza kufanikiwa na kufikia viwango vya juu vya utajiri duniani pia na wewe unaweza kufanikiwa.
Kama Nick Vujicic akiwa kwenye hali yake ya ulemavu ameweza kufanikiwa na wewe una uwezo huo wa kufanikiwa.
Una kila kitu na uwezo mkubwa wa kufanikisha kila unachokihitaji katika maisha yako.
Kuwa makini sana…usijishushe wala kujiangalia hasi hasi yaani kujiangalia hufai au kwamba huwezi kufanikiwa. Ipo nafasi kubwa ya kufanikiwa kwako tena. Hakuna kinachoshindikana ikiwa utaamua kuifungua akili yako na kubadilika.
Kama kuna sehemu umeanguka amua kuamka tena  na wala usikate tamaa. Rekebisha makosa yako, jifunze kwa wengine na songa mbele. Ishi kwa ndoto zako kila siku na jione kama msindi kwa kile unachokiendea.
Tambua mabadiliko yote unayoyataka kwenye maisha yanaanza na akili yako kwanza. Kile unachokifikiri na kukibeba sana kwenye akili yako mara kwa mara ndicho kinachotoa hatma ya maisha yako.
Kama ulikuwa unafikiri umechelewa kufanya mabadiliko katika maisha yako, haujachelewa. Anza kufanya mabadiliko kwenye akili yako kwanza kila siku baada ya muda utabadili kila kitu kwenye maisha yako na hakuna kitu cha kukushinda.
Kumbuka kama wengine wanaweza na wewe unaweza kufanikiwa pia.
Unao uwezo wa kuwa mtu wa tofauti.
Unao uwezo wa kufanikiwa.
Unao uwezo mkubwa wa kuwa nyota wa maisha yako.
Hakika unaweza, ikiwa utachukua hatua na kukubali kujifunza.
Ansante kwa kusoma makala haya na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
No comments :

Post a Comment