Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, June 14, 2017

Hapa Ndipo Chimbuko La Mafanikio Yako Linapoanzia.

No comments :
Mara zote tunakumbushwa ya kwamba ajianavyo mtu ndivyo alivyo. Miongoni mwetu tumekwisha kukataa tamaa ya maisha kabisa, wengi tumeshapoteza matumaini kwa kiwango kikubwa, hatuamini kama ipo siku ambayo tutatafanikiwa, wengi tumejiona hatuna mamlaka ya kupata kile tunachokitaka.
Na hali hii imejitokeza ndani yetu baada ya kuanza kuishi mawazo ya watu wengine, wengi tumekuwa tukiwatazama wengine hasa pale ambapo wameshindwa hivyo, kujiona ya kwamba na sisi hatuwezi. Ila ninachotaka kukwambia ya kwamba kushindwa kwa wengine liwe somo kwako ili uweza kufanikiwa zaidi.
Hii ni kwa kwa sababu hali yoyote ile ambayo inatoka nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.

Piga kazi mpaka kieleweke kuleta mafanikio yako.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Ni vyema kutafakari hivyo kwa sababu haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio basi ni lazima utafanikiwa.
Kitu kikubwa hapa unachotakiwa kujifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha.  Hii ni kwa sababu wengi wetu ni wazuri sana katika kulaum watu wengine ya kwamba wao wamesababisha wewe kuwa hivyo ulivyo leo na  inawezekana sababu hiyo ukaiona ina mashiko sana kwa upande wako, ila ninachopaswa kukwambia ni nyanyuka upya kwa kuanza kufikiri upya na pia dawa ya wapuuzi ni kuwapuuza.
Nasema hivyo kwa sababu  anakuzuia kupata mafanikio yako ni wewe mwenyewe pamoja na mawazo hasi unayozidi kuyabeba kila wakati. Narudia kusema tena uduni wa maisha yako hausababishwi   na  mtu mwingine bali wewe mwenyewe. Hivyo ni jambo lenye busara sana ambalo ni vyema kuanzia leo, amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
Hivyo ni malize kwa kusema ya kwamba huwezi kutokea kwa jirani bila kuanzia kwako, hii nikiwa na maana acha kulamu watu wengi anza kuona maisha yako mkoseaji mkubwa ni wewe ni si mtu mwingine, hata kama ni kweli mtu mwingine ndiyo sababu ya wewe kuwa hivyo ulivyo ninachotaka kukusihi ni kwamba ni tafuta mbadala wa kutatua changamoto inayokukabili na si kuwa walaam watu wengine.
Asante kwa kuwa msomaji wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio nakusihi uwashirikishe na wengine kadri uwezavyo.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,

dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment