Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, June 29, 2017

Kile Unachokiweka Kwenye Akili Yako, Ndicho Hicho Kinachokufanya Ufanikiwe Au Ushindwe.

No comments :
Kile unachokiweka ndani yako, ndicho hicho unachokitoa nje. Kama unaweka au unajirisha furaha, basi maisha yako yakatakuwa ya furaha. Kama unaingiza ndani yako hasira, basi utatoa hasira, kama pia unaweka ndani yako mafanikio, utayapata.
Jiulize, kuna wakati unakuwa na siku mbaya, siku ambayo hujisikii kufanya kitu kabisa, lakini hata hivyo ukiangalia nyuma au siku moja kabla kuna mambo ambayo uliyoyaweka akili mwako ndio yaliyokufikisha hapo ulipo.
Hata unapoona wengine wanafuraha, wanafamafanikio ni lazima ujue kuna kitu ambacho walichowekeza ndani yao na kikawapa furaha au mafanikio hayo ambayo unayaona kwa sehemu kubwa kwa nje.
Kitu unachotakiwa kuelewa, mawazo yako kila wakati yanaongozwa na hisia zako. Na hisia zako pia zinaongoza hatua unazotakiwa kuchukua, hatua hizo zinapelekea kukupa matokeo na mwisho wa siku matokeo hayo yanakutengenezea mfumo wa maisha uliokamili.

Weka mambo sahihi kwenye akili yako, ili ufanikiwe.
Kitu unachotakiwa kukumbuka, mawazo yako hayo, hayaji kwa bahati mbaya, bali yanatokana na vitu ambavyo unaviingiza akilini mwako mara kwa mara. Kwa vitu hivyo unavyoingiza ndivyo vinavyokupa mawazo hayo.
Ukijichunguza vizuri, angalia uhusiano wa taarifa unazoziweka kwenye akili yako na mtazamo wako juu ya maisha. Hapa sina shaka, utaona ni vitu vinavyofanana. Mtazamo wako ni lazima utaendana tu na yale mawazo yako.
Huwezi ukawa unaweka kwenye akili yako umbea umbea au mambo ya hovyo, halafu ukategemea kuwa na ubunifu au ukatengeneza maisha ya kimafanikio sana, hapo uwe na uhakika sana utaishia hapo hapo.
Wewe ni matokeo ya unavyofikiri. Hupendi hali ya maisha uliyonayo, hupendi sana hapo ulipo, badili sana vitu unavyoingiza akili mwako. Ukibadili vitu hivyo,hata vile unavyovitoa navyo vitakuwa na utofauti.
Kuwa na furaha, mafanikio au kuwa mtu wa hasira hasira, ni vitu ambavyo unatengeza mwenyewe na sio suala la muujiza wowote. Chunga sana kile unachokiingiza ndani ya akili yako, kumbuka hicho ndicho utakachokitoa kwa baadae.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa, endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; , +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com


No comments :

Post a Comment