Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, June 28, 2017

Sio Kila Mtu Anafaa Kupewa Kitu Hiki Cha Kimafanikio…

No comments :
Sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa, unaweza ukaweka pesa kila mfuko mwisho wa siku ukakuta katika mfuko huo hakuna kitu.  Hivyo jitahidi kuwa na mfuko sahihi kwa ajili ya kuwekwa fedha.
Mwenye utashi wa kawaida anaweza asielewe usemi huu unamaanisha nini, ila mfuko ambao ninauzungumzia ni mazingira yako yote ambayo yanakuzunguka kwa namna moja ama nyingine.
Mazingira haya ni mkusanyiko wa vitu vyote vilivyomo ndani yake ikiwemo na mwanadamu mwenyewe. Na mwanadamu huyu ndiye mwenye uwezo wa kufanya mazingira hayo yaweze kuwa bora au mazingira hayo kwa namna moja ama nyingine.
Sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa. Katika safari yako ya kuelekea mafanikio makubwa, si kila mtu anafaa kumwambia jambo ambalo unalitaka kulifanya. Nasema hivi kwa sababu wengi wetu tumekuwa hatuwashirikishi watu sahihi katika mambo ambayo tunatamani kufanya, mwisho wa siku tumekuwa watu ambao maisha hayo tunayona machungu kama alovera.

Sio kila mtu anafaa kuambiwa kila kitu.
Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya ili uweze kuwa bora na kufanikiwa zaidi, unachotakiwa kufanya ni kutafuta watu sahihi kwa kile ambacho unakifanya au kwa kile ambacho unataka kukifanya. Ukiwa na upele hakikisha unamtafuta mtu mwenye kucha, kwani endapo utamtafuta mtu ambaye hana kucha ni sawa ni kutwanga maji katika kinu.
Kama unataka kufanya biashara ya kuuza mchicha usiende kuomba ushauri kwa muuza mkaa kwani hatakuwa na ushauri wa kutosha kuhusu biashara ya mchicha zaidi atakupa maoni binafsi kwa kile ambacho anakiona kwa wafanyabiashara wa mchicha. Na mwisho wa siku atakwambia biashara hii haifai. Hivyo kwa kila chochote unachotaka kufanya hakikisha unafuta mtu ambaye anakifahamu kitu hicho kwa undani zaidi.
Hata wewe ndugu yangu mwenye siri ndani ya moyo wako, epuka kumwambia kila mtu hiyo siri yako kwani wapo  wengine katika dunia hii, wapo kwa ajili ya kusambaza siri za wengine. Hivyo jitahidi sana wewe mwenye siri nzito ndani ya nafsi yako, epuka kuweka pesa kila mfuko kwani mifuko mingine ni mapambo.
Pia kama wewe ni kiongozi wa serikali au kampuni binafsi, nawe nakwambia sio kila mfuko unafaa kuwekwa pesa. Kama unataka kufanya uchaguzi wa mtu fulani ambaye anafaa kusimamia ofisi yako, hakikisha unafanya uchunguzi sahihi kabla kumchagua mtu fulani. Kufanya hivi kutakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuja kujutia maamuzi yako.
Mwisho ninamini umenielewa vyama ya kwamba si kila mfuko unafaa kuwekwa pesa.
Ndimi Afisa mipango wa mafanikio, Benson chonya,
0757 90 99 42,                                  
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment