google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 12, 2017

Ifahamu Misingi Hii Ya Kuilea Ndoto Yako ili Uweze Kufanikiwa.

No comments :
Katika ulimwengu huu wa teknolojia kila mmoja wetu ana ndoto yake, na kila miongoni mwetu anatamani siku moja ndoto iwe kweli. Ila changamoto kubwa huwa inakuja ni kwa jinsi gani unaiweza kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli. Wengi wetu ndoto zetu ni za mdomoni tu, huwa hazina uhalisia wa jinsi ya kuzikamilisha ndoto hizo.
Lakini siku zote ikumbukwe katika safari ya mafanikio, kuwa makini sana na jinsi unavyoitunza na kuilea ndoto yako. Kama ndoto yako unaitunza na kuilea katika hali ya hofu na mashaka sana basi, utavuna magugu na hautaweza kufanikiwa.
Wengi wetu tumekuwa tumeweka mitazamo hasi juu ya ndoto zetu, wengi tumekuwa tukiyatazama mambo katika mtazamo hasi, wengi tumekuwa hatujui namna na jinsi ya kuzitimiza ndoto zetu. Kwa mfano, unaweza ukakuta mtu anatamani kuwa mfanyabiashara fulani, lakini cha ajabu ukimuuliza mtu huyo ni mikakati gani ambayo amejiwekea ili kukamilisha ndoto yake hiyo, utakuta hakuna mkakati hata mmoja.

Lea ndoto yako katika msingi mkubwa wa kujiamini, utafanikiwa.
Najaribu kujihoji kwa sauti ya nne, hivi kwa kufanya hivyo ni kuijenga ndoto yako au ni kuibomoa? Bila shaka kufanya hivyo ni kuibomoa ndoto yako na hatimaye kujiandalia makazi ya kiumaskini.
Lakini ukweli ni kwamba ili uweze kutimiza ndoto yako unatakiwa kuitunza na kuilea ndoto hiyo katika misingi ya  imani na matumaini makubwa ya kimafanikio, lakini pia ni lazima uweze kujiamini kila wakati, hii ni kwa sababu wapo wengi wanaoshindwa kufikia ndoto zao kwa sababu ya kuzielea ndoto zao katika mazingira mabovu.
Kama ulivyo mmea ili ukue ni lazima umwagaliwe maji safi, halikadhalika ndoto  yako iko hivyo hivyo. Ni lazima ndoto yako ituzwe kwa matumaini na imani ya mafanikio na sio kuitunza katika hofu na woga ambapo mwisho wa siku ni lazima utakwama.
Hivyo kwa kuwa wewe ndiye mmliki wa ndoto yako hakikisha unaweka mikakati imara ambayo itakufanya uweze kufika pale ambapo unapopataka, kwani endapo utafanya kinyume chake ni kushindwa kutimiza  kutimiza kusudio lako hapa duniani.
Hivyo kila wakati jaribu kutafakari juu ya mambo haya;
Najua hapo ulipo una ndoto ya aina fulani, jiulize
Unailea ndoto yako katika mazingira yapi?
Je, unajiamini  ya kwamba utafanikisha ndoto yako?
Au  upo kwenye mazingira ya mashaka na hofu?
Lakini ikumbukwe ya kwamba mazingira yoyote yale unayoyatumia kuilelea ndoto yako yanakupa jibu kama utafanikiwa au hautafanikiwa kuifanikisha ndoto yako. Hivyo ni vyema ukatafakari kuhusu mazingira uliyopo kwa sasa kama ni kweli ndoto yako itatimia au haitatimia.

Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
bensonchonya23@gmail.com,
dirayamafanikio.blogspot.com
.


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.