google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 19, 2017

Namna Unavyoweza Kuishi Katika Ulimwengu Wa Wakatishaji Tamaa.

No comments :
Dunia ya leo imejaa maneno mengi kuliko watu waliopo katika dunia hiyo. Hebu fikiria ya kwamba tafiti za wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza maneno 16000 kwa siku, wakati wanaweke wote duniani kwa kila mmoja mmoja huzungumza maneno 25000 kwa siku, kwa tafiti hizi najaribu kuwaza  hivi tuna watu wangapi? Na kila mmoja akizungumza maneno yake tutakuwa na maneno mangapi?
Najaribu tu kuwaza kwa sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya watu. Nasema hayo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi  katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyohivyo  sawa na kusema.
Hata hivyo maneno ya watu ambayo yapo katika dunia hii ni yale ambayo yanatengeneza ulimwengu mpya, ulimwengu huo huitwa ulimwengu wa taarifa, katika ulimwengu huo yapo mengi ambayo utayasema na mengine utayasikia, na katika ulimwengu huohuo taarifa hizo hizo ambazo utakuwa unazisikia, yapo yale yatakayokujenga, lakini yapo yale ambayo yatakufanya uvurugike kabisa.


Na ukweli ni kwamba maneno ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson hii ni kwa mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa zimejaa tarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele kimaisha.
Na mara kadhaa hali  hii hutokea  na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe. Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa wewe jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, tunachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba  acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia kuendesha maisha yako, kwa sababu kama ukifanya hivyo utaumia sana na utaiona dunia chungu.  Hivyo ni vyema ukaamua kuishi wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma kukufanya. Kufanya hivyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
Tumalizie kwa sema ya kwamba endapo utamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza wakatishaji tamaa katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku zote za maisha yako. Lakini pia faida nyingine ambazo utazipata pale ambapo utamua kuishi maisha ya kujitolea hukumu, utakuwa na uhuru mkubwa katika kutoa maamuzi yako.
Asante sana kwa kuwa nasi, tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
dirayamafanikio.blogspot.com.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.