Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, June 25, 2017

Jitoe Kikamilifu Na Boresha Maisha Yako Kila Siku Hivi…

No comments :
Hitaji lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea yaani learn, grow and develop. Hili ndio hitaji lako la kwanza.
Kila wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au hicho unachokifanya ili kuleta matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo na hata kesho ili kikupe mafanikio
Unaweza ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha tabia, biashara au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi. Unapoboresha kila eneo unajikuta ndio unazidi kufanikiwa.
Kuendelea kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako, kila siku jiulize, ni kwa namna gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha maisha yako yakawa bora kuliko jana?

Jifunze kila wakati kufikia mafanikio yako.
Kufanya mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda (Becoming a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili kuwa mbobezi kwa hicho unachokifanya.
Hakuna mpaka wa kuboresha maisha yako. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha  yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa tena kwa viwango vya juu.
Lakini mafanikio hayo ninayaongelea hapa hayawezi kuja  kama upepo wa kipunga au hayawezi kutokea usiku eti umelala na ukiamka ukawa tajiri, kumbuka inachukua muda hadi mafanikio yako kujengeka.
Kuwa mvumilivu katika kipindi ambacho ndoto zako zinapitia kwenye mchakato wa kuelekea kufanikiwa, vinginevyo hautaweza kufanikiwa kwa kitu chochote zaidi utaendelea kuacha ndoto zako nyingi zikiwa hewani.
Kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha, fanya iwe ndio kanuni kuu ya maisha yako. Kwa wenzetu wa Japan kanuni hii wanaiita KAIZEN. Hio ikiwa na maana wao hujifunza sana katika hili la kuboresha maisha  yao kila siku.
Wajapan wakiwa tokea vijana wadogo wanajifunza juu ya hili na kuchukua hatua za kuboresha maisha yao na limejenga na kuwa utamaduni mzuri ambao kila mtu anaufuata kwenye maisha yao.
Hata wewe huhitaji kulala, angalia kila eneo la maisha yako ambalo haliko  sawa, amua kuliboresha kwa guvu zote na kwa bidii kila siku. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Chukua hatua kwa kufanyia kazi haya uliyojifunza leo yawe sehemu ya maisha yako.
 Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.comNo comments :

Post a Comment