Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, June 26, 2017

Hiki Hapa Ndicho Kinaongoza Mafanikio Yako.

No comments :
Kitu kinachoongoza matendo yako au hatua za namna fulani unazochukua kwenye maisha yako ni zile picha unazoweka kichwani mwako jinsi unavyotaka maisha yako yawe. Huwezi kuchukua hatua kubwa kama picha ulizonazo ni kidogo.
Ndio maana, kila wakati tunasisitiza ni muhimu sana kuwa na picha sahihi, maana picha hizo zitakuongoza pia kuchukua hatua sahihi. Hebu jiulize hapo, picha ulizoweka kichwani mwako kila wakati ni zipi?

Je, unaona nini kwenye maisha yako? Unaona kufanikiwa au unaona kushindwa? Kama unaona kufanikiwa, uwe na uhakika ni lazima utachukua hatua kubwa sana za kukufikisha kule unakotaka kufika.
Kila wakati, jitahidi kuongozwa na picha sahihi za mafanikio unayoyataka, ili picha hizo zikusaidie pia kuchukua hatua kubwa. Hatua anazochukua mtu kwenye maisha yake, ni ushahidi tosha kwa mtu huyo ana picha gani kichwani mwake.
Huhitaji kupiga ramli, huhitaji muujiza wowote ule. Ukitaka kujua mtu huyo anawaza nini juu ya maisha yake au atafika wapi kimaisha, angalia hatua anazochukua, hizo zitakuonyesha mtazamo na picha alizoweka kuhusu maisha yake.

No comments :

Post a Comment