Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, June 6, 2017

Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo - 2.

No comments :
Wiki iliyopita tuliona mara baada ya mama mjane kumualika mfalme Mhavila nyumbani kwake na kukubaliwa, lakini alimsubiri sana Mfalme hakutokea,na akajikuta amegawa chakula kwa mfalme kwa watu wengine, akiwa katika kusubiri huko ghafla alisikia hodi.
Mama mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme Mhavila akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini mfalme Mhavila kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme Mhavila alifika kwa mama mjane na  kusema asante sana kwa kunijali.
Mama mjane aliwaza na kusema mfalme Mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati sijamfanya chochote? wakati mama akitafakari amemjali kwa lipi mfalme Mhavila mama mjane hakupata majibu, lakini pili mama mjane aliwaza katika halmashauri yake ya kichwa atampa chakula gani, na ili hali chakula kulikuwa kimekwisha chote.
Wakati mama mjane unawaza kwa kweli hakupata majibu, zaidi ya maswali lukuki yaliyokuwa yakizidi kumiminika katika akili yake. Kabla hajapata jibu hata moja katika maswali yale ambayo alikuwa anajihoji, aliwaza tena iweje tena mfalme Mhavila kachelewa kiasi kile, lakini alizidi kuwaza imekuwaje mfalme Mhavila kaja na watu lukuki kiasi kile huku wakiwa katika hali ya furaha kiasi kile?

Wakati maswali hayo yote yakiwa katika halmashauri yake ya kichwa cha mama mjane pasipo majibu yake, mfalme Mhavila alimuamuru mama mjane waingie ndani kwake mama mjane kwa ajili ya kufanya mazungumzo kidogo, wakati mama mjane akiwa haelewi ni nini cha kufanya, basi aliingia ndani kwa ajili ya kumsikiliza mfalme Mhavila, japo mama mjane aliwaza atampa nini mfalme Mhavila kwani chakula kilikuwa kimekwisha liwa na watu wengine ambao walijitokeza mchana.
Basi ikawa asubuhi ikawa jioni, wakafika ndani kwa mama mjane, mfalme Mhavila akarudia tena kumshukuru mama mjane kwa kusema asante sana kwa kunijali, pia asante kwa kushiriki kwa pamoja kwa chakula chako cha mchana ambacho tulikula kwa pamoja kwa kweli kilikuwa kitamu sana asante sana mama.
Mama mjane akafungua kinywa chake huku akiona aibu, iliyojawa na mshangao,  kwa kula chakula? Chakula kipi mfalme? mama mjane alihoji, huku akizidi kusema wakati mimi nilikusubiri hakufika na chakula nimekigawa chote.
Alipomaliza kuweka nukta mama mjane , mfalme Mhavila naye akadakia oooh usijali mama wale watu wote walikuja kula chakula pamoja na maji niliwatuma mwenyewe, hata hivyo nilifanya vile kwa maksudi kabisa, ili kuona una huruma kiasi gani cha kutoa kwa watu usiwajua? Hivyo majibu ambayo nimeyapata yamenipa picha nzuri sana, ambayo kimsingi nimeelewa sana ni kwa jinsi gani ulivyo mkalimu.
Kama uliweza kuwatendea vema vijana wangu wale usiowajua, nina imani moyo na hali uliyonayo wewe ni mkalimu sana. Hata hivyo nichukue fursa hii kukushukuru tena kwa mara nyingine kwa ukalimu wako. 
Wakati mfalme Mhavila anasema hayo, mama mjane alishangaa sana, kumbe wale vijana na yule mtoto walikuwa wametumwa na mfalme? Mama mjane aliwaza katika fikra zake. 
Mfalme akaendelea kusema "Hivyo kwa ukalimu ulionao inaonesha dhahiri shairi ya  kwamba wewe ni kiongozi bora! Kwani binafsi naamini ya kwamba kiongozi bora ni yule aliye mkalimu na mwenye huruma kwa watu wake.
Hivyo nakushukuru sana, na kwa kuwa ulisema ya kwamba wewe ni mjane, nitakupa mtaji wa sh. Milionio mia moja kwa ajili ya kufungua miradi yako, na mradi ambao natamani ufungue ni ule ambao utawasaidilia watoto waishio katika mazingira magumu hususani watoto yatima!
Nitakupa watalam mbalimbali ambao watakusidia katika kukamilisha mpango huo, lakini pia nitakutafutia wawekezaji ambao  watakusaidia katika jambo hilo.
Baada ya dakika chache mama mjane alimshukuru mfalme Mhavila kwa kumpa wazo bora pamoja na fedha katika kuwasaidia watoto. Mfalme Mhavila akamuuliza mama je, unadhani ni jina gani linafaa kwa ya mradi huo?
Mama mjane aliwaza kidogo kisha akasema jina ambalo linafaa katika mradi huo ni "mama mjane foundation" . Mfalme Mhavila hakuwa na kipangamizi juu ya jina hilo hivyo walikubaliana libaki kama lilivyo. Hapo ndipo mwanzo wa kubadilika kwa maisha ya mama mjane.
Mwisho mfalme Mhavila akamuahidi mama mjane kwamba utekelezaji wa jambo hilo ungeanza kufanyika mara moja! Hivyo naamini ya kwamba hutaniangusha katika hili, kwani naamini utafanya ‘wonders,’ wazungu husema hivyo. Basi kabla mfalme  hajaondoka mama mjane akamshukuru tena katika mambo mbalimbali ambayo walikuwa wameongea.
Lakini pia mama mjane akampa mbinu nyingine ambayo ni njia bora sana mfalme ambayo ingesaidia katika kuleta mafanikio katika jamii ile. Mama mjane akasema mfalme uongozi ni karama kutoka kwa Mungu wetu, hivyo kwa kila kitu unachokifanya hakikisha unamshirikisha Mwenyezi Mungu, lakini pia hakikisha unawashirikisha wananchi mbalimbali katika kutenda mambo mbalimbali ya mafanikio, kwani kukaa pekee yako na kufanya maamuzi haisaidii kwani maendeleo ni ya watu wote! Hivyo kuwashirikisha watu ndiyo mbinu bora zaidi ya kupata mafanikio na maendeleo  yenyewe.
Mwisho mfalme akafurahi kusikia kwa ushauri kutoka kwa mama mjane, wakaagana huku siku chache utekelezaji ukifuata.
Mwisho; Umejifunza nini kutokana na hadithi hii, tuma ulichijifunza kupitia 0757-909942. Kwa kuanza na jina lako na mahali ulipo nasi tutaweka maoni yako hapa wiki ijayo siku kama ya leo.

Ni wako katika ujenzi wa mafanikio; Benson chonya,
bensonchonya23@gmail.com
0757909942
dirayamfanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment