google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 15, 2018

Habari Njema Na Kubwa Ya Kimafanikio Kwa Zama Hizi Ni Hii Hapa.

No comments :
Habari njema  katika zama hizi ambazo tunazo ni kwamba, yapo mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa, zipo fursa nyingi ambazo zinatikiwa kufanywa, kikubwa kwako ni kutuliza akili yako sana na kuamua kufanya fursa moja tu ambayo umeichagua.
Hata kama kuna wakati unajihisi kama umechanganyikiwa vile, yaani nikiwa na maana unajiona huna cha kufanya, kitu cha kufanya tuliza akili yako, na chagua fursa moja makini na matata kwako ifanye na acha kutangatanga kwani fursa zipo za kutosha.
Kitu cha msingi kwako sasa, zingatia ile hatua ya kwanza, fanya kitu sasa, chukua hatua ya kwanza katika utendaji. Kuongea sana usiendelee kuongea, wewe ongelea kwenye hatua na hilo litakusaidia kusonga mbele sana kuliko unavyowaza.

Kama unaona kwako ni shida kuanza, anza na hatua ndogo kabisa, kama wewe ni mwandishi anza na kuandika sentensi ya kwanza, kama unataka kufanya biashara anza na mteja wa kwanza, chochote kile anza na kidogo.
Kama ni kukaa, umekaa vya kutosha yaani ukiwa unasitasita kwa kutokujua hujui nini cha kufanya. Chagua kitu chochote na anza kukifanya kitu hicho mara moja, kwani kama nilivyosema zipo fursa nyingi za kufanya kwa nyakati hizi uamuzi ni wako.
Pia uelewe fursa hizo zipo za kila aina ya mtaji, zipo fursa za mtaji mdogo kabisa na zipo fursa unaweza ukaanza nazo ambazo hata hazina mtaji ni wewe tu kuamua kuzichangamkia na kuzifanya mara moja.
Kama bado unazile fikira za kuanza biashara na mtaji mkubwa sana  unajichelewesha, wewe anza na mtaji mdogo tu na kwa kuanza huko utaendelea kukua polepole na mwisho utafika utafanikiwa kwa viwango ambavyo unavyotaka.
Lengo la makala haya si kukutajia fursa hizo, bali ni nikukumbusha kwamba upo kwenye kipindi ambacho kina fursa nyingi tena na za kutosha. Najua wewe ni shahidi kwenye hilo na unaona fursa hizo kwenye maisha zinavyokuzunguka.
Ili uweze kuzifaidi fursa hizo huhitaji kutoa sababu, fanya chochote hata kama ni kidogo. Upo kwenye kipindi ambacho una fursa kibao na unatakiwa kipindi hicho ukitumie vizuri ili kuweza kufanikiwa kwa kutumia fursa hizo kikamilifu.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.