google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 26, 2018

Jinsi Unavyoweza Kuboresha Maisha Yako Hatua Kwa Hatua Kila Siku.

No comments :
Kuboresha maisha yako kila siku na kwa kidogo kidogo ni jambo la muhimu sana kwako kuliko kuharibu maisha yako kila siku hata kama ni kwa kidogo pia. Kuboresha maisha yako kila siku ni jambo la muhimu sana kulifanya.

Unapoanza kufikiria juu ya kuboresha maisha yako, acha kuwaza juu ya kuchukua hatua kubwa sana itakayoleta matokeo ya ghafla na ya kushangaza  wengi. Unachopaswa kufikiria ni kuleta mabadiliko ya kila siku hata kama ni kidogo.

Kwa mfano, kubadilisha maisha yako kwa asilimia moja kla siku ni kitu ambacho unaweza usikione kina faida, lakini ukifanya mabadiliko hayo kila siku na kwa muda mrefu mabadiliko hayo huanza kuonekana tena kwa uwazi.

Hapo unaona kilicholeta utofauti ni yale mabadiliko kidogo kidogo na maamuzi kidogo sana na ndivyo unabadilisha maisha yako na kuwa ya tofauti na kuwaacha watu wengine wakikushangaa eti ulifanyaje hadi hayo yakatokea.

Kama kuboresha maisha yako kila siku ni jambo la mujimu na ambalo linaweza kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio, je, ni kitu gani kifanyike ili uwe na uhakika wa kuweza kuboresha maisha yako hatua kwa hatua na kila siku.


1. Fanyia kazi zaidi mambo yaletayo matokeo chanya.

Usijajidanganye kufanya mambo ambayo hayakupi matokeo mazuri. Yale mambo yanayoleta matokeo mazuri yafanye zaidi. Hata kwenye mpira kikosi kinacholeta matokeo bora hicho ndicho kinachopangwa kila wakati.

Kaa chini na angalia ni mambo gani ambayo yanaleta matokeo mazuri kwako na yafanye mambo hayo kila siku. Nasema hivi, usipoteze muda wako kufanya mambo ambayo hayakupi matokeo chanya, utakwama, kabisa.


2. Epuka kufanya makosa madogo madogo yasiyo ya lazima.

Unaweza usione matokeo yake kwa sasa, lakini makosa madogo madogo yanaathari kubwa sana katika kujenga au kuharibia maisha. Unatakiwa kujua kuepuka kupoteza pesa ndogo ulizonazo, muda kidogo ulionao na kila siku.

Kwa kadri jinsi unavyomudu kuepuka kufanya makosa madogo madogo, ambayo kwa dhahiri hayawezi kukupa matokeo chanya, ndivyo unajikuta upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa. Makosa madogo au ‘tinny losses’ ni lazima kuyaepuka.


Kwa kuepuka kufanya mambo yasiyo leta matokeo na pia kuepuka kufanya makosa madogo madogo kila siku utajikuta unaboresha maisha yako na mwisho wa siku utajikuta unatengeneza maisha yako na kuwa bora zaidi na zaidi.

Kikubwa ambacho unatakiwa kukumbuka hapa, ni kuamua kuvaa jukumu la kuboresha maisha yako kila siku. Ukiamua kuboresha maisha yako na kwa kila siku uwe na uhakika utafanikiwa hata kama mabadiliko hayo hayaonekani leo, kesho yataonekana.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.