google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 20, 2018

Yajue Mambo Ya Muhimu Katika kurahisisha Safari Ya mafanikio Yako.

No comments :
Shughuli zote zifanywazo na mwanadamu katika sayari hii ya dunia, kila mmoja baada ya kufanya shughuri hilyo ni lazima mtu huyo anategemea kupata pesa, unashangaa wala usishangae huo ndio ukweli halisi. Na miongoni mwa siri ambayo hujawahi kuijua kuhusu mafanikio ni kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya ni lazima uwaze kwa kina kitu hicho kinakuing’iziaje pesa?
Hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu hufanya vitu visivyo vya msingi hii ikiwa ni kigezo cha  kuiburudisha  nafsi basi jiandae kupata tabu sana. Nimesema hivyo kwa sababu mambo yamebadilika sana hivyo habari za kuufariji moyo katika jambo unalolifanya pasipo kuingiza kitu chochote katika maisha yako kunajipoteza mwenyewe.

Lakini pia unatakiwa kufahamu ya kwamba Maisha yako ni mjuimuko wa mambo madogo madogo ambayo wewe kama dereva unapaswa kuyafahamu vyema mambo hayo ili kuhakikisha maisha yako yaweze kusonga mbele kimafanikio, au kwa maneno mengine siku zote ni lazima ufahamu ya kwamba hatma ya maisha yako unayo wewe na si mtu mwingine.
Pia ikumbukwe ya kwamba unavyoonekana hivi leo ni matokeo ya kwako mwenyewe ndiye uliyeamua kuwa hivyo ulivyo, usiruhusu nafsi pamoja na kinywa chako kumlam mtu mwingine kukusababishia ugumu wa maisha, kwani nimeshasema hapo awali ya kwamba wewe ndio dereva halisi wa maisha yako na si vinginevyo.
Wewe ndiye mwenye maamuzi sahihi ya kufanya jambo fulani au usifanye. Mara nyingi watu wengi sana wanashindwa kukidhi matakwa ya maisha yao kwa sababu wameruhusu watu wengine ndio wawe waamuzi wa kile wanachokifanya na kitendo hiki ndicho kinachowapeleea watu hawa wazidi kulalama maisha ni magumu, na kitendo hiki ndicho kinachotupoteza wengi.
Vile vile watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wao pia wameshindwa kufanikiwa katika maisha yao hii ni kwa sababu wameshindwa pia hata kuchagua hata marafiki sahihi wanaopaswa kuongozana nao katika maisha yao.
Ni ninii kinatakiwa kufanyika ili kuishi maisha yenye tija katika safari hii ya dunia katika kuyasaka mafanikio?
Mosi,  unachopaswa kukizingatia katika dunia hii ili uweze kuishi maisha ya mafanikio ni kuhakikisha unakuwa ni mtu mwenye maamuzi  yako sahihi ambayo yatakufanya uweze kutimiza kusudio lako hapa duniani ili mradi usivunje sheria za nchi na sheria za Mwenyezi Mungu.
Jambo la pili, kwa kila jambo unalolifanya ni vyema ukawa ni mtu wa kujiuliza hivi jambo hili lina manufaa yeyote yale kwangu? Na je napateje pesa kupitia jambo hili?
Jambo la tatu na la mwisho, ni vyema ukajifunza kuchagua marafiki sahihi wataokusaidia kupiga hatua za kimafanikio za kule ambako unataka kuelekea na si vinginevyo.
Kwa leo sina mengi, naomba niishie hapo nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango; Benson Chonya


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.