google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 27, 2018

Huu Ndio Ukweli Unaouma Utakaofanya Maisha Yako Yawe Bora.

No comments :
Ni jambo la kawaida kwa watu wengi kuwa na ndoto na malengo, lakini ipo tofauti kubwa sana kati ya watu ambao wanafanikisha malengo yao na wengine wanashindwa kufanikisha malengo yaani hawa wanakuwa wanaota tu pasipo kufikia malengo.
Kwa nini hali hii inakuwa inatokea wengine wanakuwa na uwezo wa kufanikisha malengo yao na wengine wanakwama kufanikisha? Hapa ndipo unatakiwa ujue ukweli mgumu, ukweli unaouma ambao utafanya maisha yako yawe bora.
Je, nikuulize hapo ulipo upo tayari kuupokea ukweli mchungu ambao utabadilisha maisha yako? Kama uko tayari nyosha mkono, nikupe ukweli huu, ila mara baada ya kupokea ukweli huo, utakusaidia sana kukubadilisha maisha yako kwa ujumla.

1. Hatua ya kwanza ni ngumu kutekelezeka.
Inaeleweka siku zote ili kufanikisha jambo lazima kuchukua hatua. Hata hivyo kwa bahati mbaya sana siku zote hatua ya kwanza mara nyingi inakuwa ni ngumu sana kuweza kutekelezeka. Kama usipoweka juhudi na kujituma sana huwezi kuchukua hata hatua ile ya kwanza. Kuna watu wanakuwa wanakwama hata kabla hawajachukua hatua ya kwanza. Fanya ufanyalo, tumia nguvu zote na kuhakikisha unaanza.
2. Wewe ndie sababu ya kujirudisha nyuma sana.
Hakuna mtu mwenye mchango mkubwa sana wa kukurudisha nyuma zaidi yako. Unajirudisha nyuma kutokana na hofu ambazo unazo, unajirudisha nyuma kwa sababu ya kushindwa kuchukua hatua mapema na pia unajirudisha nyuma kwa sababu ya visingizio. Unatakiwa uyaepuke haya yote ili ufanikiwe.
3. Mambo makubwa yanataka muda na juhudi ili kuyafanikisha.
Hakuna jambo kubwa ambalo unaweza ukalifanikisha kwa haraka na upesi kama unavyotaka. Siku zote mambo makubwa yanataka muda na juhudi kubwa sana ili yaweze kutimia. Kama una haraka zako na hutaki kuweka muda katika kutimiza makubwa, utaishia kupata vitu vidogo sana maishani mwako.
4. Sio kila mtu yupo tayari kukusaidia.
Pamoja na kwamba unaweza ukaona unazungukwa na watu wengi wema, lakini nikwambie tu unapopata changamoto si kila mtu yupo tayari kukusaidia kufanikiwa na kufika juu. Wapo wengine watakudidimiza chini na hutaamini, ili usitape tabu weka akilini hii, si kila mtu yupo tayari kukusaidia kama unavyofikiri wewe iko hivyo.
5.  Huwezi kufanikiwa bila kujitoa mhanga.
kama unafikiri utafanikiwa tu kirahisi pasipo kuhatarisha baadhi ya mambo basi utakuwa ni mtu ambaye unajidanganya sana. Lazima ifike muda au wakati uhatarisha baadhi ya vitu kwa ajili ya mafanikio yako. Hatari haziwezi kutoka kabisa ila kama unafikiri mafanikio ya namna hiyo yapo huwezi kuyapata katu maishani.
6. Huwezi kutawala kila kitu.
Ukweli huu unakuja hasa pale unapotaka kutawala tabia na matendo ya watu. Huwezi hata siku moja kutawala tabia na matendo ya watu. Vipo vitu unavyoweza kutawala lakini si kutawala tabia zao na ukazimiliki kwa jinsi wewe unavyotaka iwe. Tawala yale unayoyaweza lakini si kutawala kila kitu utashindwa na hautaweza kufanya hivyo.
7. Huwezi kufanya kila kitu mwenyewe.
Kama ambavyo huwezi kutawala kila kitu wewe, basi huwezi kufanya kila kitu mwenyewe. Yapo majukumu inabidi uwaachie watu wakusaidaie, vinginevyo ukiwa wewe kama wewe yatakushinda. Wale wanaong’ang’ania kufanya mambo yao peke yao wanashindwa kutoka au kuweza kufanikiwa kabisa kwa sababu ni ngumu hiyo.
8. Kukosea ni lazima.
Huwezi ukafanya jambo lolote pasipo kufanya makosa. kukosea ni lazima kutokee kila wakati unapoelekea ndoto zako. Na kunapotokea kukosea kwa namna yoyote usichukie, amua kujifunza kupitia kukosea huko ambako unashindwa na si kuchukia na kuona kila kitu ndio kimeishia hapo na huwezi kufanikiwa tena.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.