google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 14, 2018

Kipande Muhimu Unachopaswa Kuunganisha Katika Maisha Yako Ili Uweze Kufanikiwa Ni Hiki.

No comments :
Neno maisha ni mkusanyiko wa viapnde vidogodogo ambavyo vimetawanyika na pindi vikusanywapo kwa pamoja hutengeneza kitu kinachoitwa mafanikio. Na moja ya sababu kubwa ya wengi wetu kushindwa kufikia kilele cha mafanikio hayo ni kwamba tumeshindwa mbinu madhubuti ya kukusanya vipande hivyo na kuviweka pamoja  ili tuweze kufanikiwa.
Leo nitakueleza ni kipande ambacho ni muhimu  unachopaswa kukiunganisha katika maisha yako  ili uweze kufanikiwa kiurahisi, Kwani wengi wa watu ambao wameweza kufanikiwa katika sayari hii ni kwamba waliweza kufanikiwa kipande hiki hatimaye kuweza kufanikiwa.
Kipande hicho si kingine bali  ni unahitaji mtandao wa watu ili uweze kufanikiwa. Moja kati ya changamoto kubwa ambayo ipo na inaendelea kutuua taratibu ni kwamba hatuna watu sahihi ambao wanasabisha sisi kuweza kusonga mbele katika harakati za kufanikiwa.
Wengi wetu, watu tulionao ni wale wale wa siku zote ambao ukiwambia unataka kufanya jambo fulani lenye tija ni lazima watu hao watakuleleta sababu za kushindwa tu. Watu wa aina hii hawafai hata chembe na vyema kuwaepuka mapema.

Watu sahihi na wenye malengo na mitizamo chanya ndio wanaotakiwa kuyazunguka maisha yako ya kila siku iwe ni kwa kupenda au kwa kutokupenda.
Hebu fanya zoezi dogo shika simu yako kisha pekua majina ya watu mbalimbali waliopo katika simu yako, je majina mangapi yana manufaa/msaada  kwako? Jibu baki nalo.
Nimukuuliza swali hili kwa sababu asilimia 99.999 wengi wetu simu zetu zimejaa majina ambayo hayana chachu yeyote katika kuhakikisha tunapiga hatu za kimafankio.
Nini kifanyike; Ukiona simu yako haina majina matano ambayo yanachangia kitu chochote kwenye maisha yako basi simu hiyo iweke kwenye maji kwani haina umuhimu wowote kwako (hapa nimetia chumvi).
Ila ukweli ni huu, Unachotakiwa kufanya ni kwamba katika maisha yako ya kila siku hakikisha ya kwamba unazungukwa na watu chanya wenye kuchangia jambo fulani katika maishha yako ya kila siku. Kama ni marafiki basi chagua marafiki ambao  mtashauriana mambo chanya na yenye kuleta tija katika maisha yako na si vinginevyo.
NUKUU YA LEO; Mtandao wa mafanikio wenye watu chanya, ni  njia ya kufikia kilele cha mafanikio yako (by Benson Chonya)
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku mwema na utume mwema, asante
Benson chonya
0757909942 .

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.