google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 29, 2018

Faida Tatu Muhimu Za Kuchukua Hatua Kwa Kile Unachotaka Kukifanya.

No comments :
Ili kufikia mafanikio yako, kuwa na mipango mizuri au mikakati iliyobora ni jambo zuri sana ikiwa kama utachukua hatua. Kama usipochukua hatua mipango yako hiyo mizuri haitasaidia kitu itakuwa ni sawa na kazi bure.
Kitu cha msingi kwako ili mipango yako ieleweke ni kwa wewe kuchukua hatua mapema za kukusaidia kuweza kutimiza ndoto zako. Zipo faida za wewe kuchukua hatua kwa kile unachotaka kukifanya, haijalishi umefanikiwa kwa jambo hilo au hapana.
Elewa hivi, mbali na faida kubwa ya kufanikisha lengo husika la kile unachotaka kukifanya, lakini zipo faida nyingine tatu muhimu, ambazo tu wewe utazipata kama utachukua hatua ya kufanya. Faida hizi huwezi kuzipata au kuziona mpaka uchukue hatua.

1. Utawajibika zaidi.
Kile kitendo cha wewe kuchukua hatua tu, kitakufanya wewe kuwa mtu wa kuwajibika zaidi tofauti na ambavyo kama usingeweza kuchukua hatua. Najua hutataka mambo yako yaende hovyo ila utawajibika na kujituma sana ili ufanikiwe.
Hiki ndicho kitu cha kwanza au faida ya kwanza ambayo utaipata endapo utachukua hatua. Utashangaa jinsi unavyopata shauku ya kuendelea kutaka kufanya zaidi na zaidi ukumbuke yote hayo hayaji kwa bahati mbaya ila ni kwa wewe kuchukua hatua.
2. Utajifunza kutokana na makosa.
Hauwezi kujifunza kutokana na makosa kama haujachukua hatua. Kuchukua hatua ni lazima ili ujifunze kutokana na makosa yako yaani ujue ni wapi ulipokosea na ni wapi unatakiwa kupaboresha zaidi na zaidi hadi uweze kufikia lile lengo lako.
Wengi wanaoshindwa kufanikiwa sana hawachukui hatua na ni watu wa kusitasita sana na kwa sababu hiyo inawafanya washindwe kujifunza kutokana na makosa yao. Chukua hatua leo, uone jinsi utakavyojifunza kutokana na makosa yako.
3. Utapata msaada wa ziada.
Kutokana na kile ambacho umeamua kukifanya na umeamua kuchukua hatua, hiyo itakusaidia sana kuweza kupata msaada kwa watu wengine ambao hukutegemea. Msaada huo huwezi kuupata kama umejikalia tu na huchukui hatua.
Kama unafikiri nakutania chukua hatua leo, halafu uone kama utakosa watu wa kukusaidia kwa lile lengo lako. Unakosa watu wa kukusaidia kufanikisha kwenye lengo lako kwa sababu hujachukua hatua. Ukichukua hatua watu hao utawapata.
Hizi ni faida tatu nyingine muhimu ambazo utazipata kama utachukua hatua ya kufanya jambo lile unalotaka kulifanya. Je, hapo ulipo unasubiri nini kuchukua hatua. Chukua hatua za kuwajibika ili utimize ndoto zako mapema.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.