google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 27, 2021

Silaha Kubwa Ya kufikia Mafanikio Yako Ni Hii.

No comments :

Kati ya kitu muhimu sana cha kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Kati ya silaha kubwa ya kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Unapokuwa na akili ya utulivu inakusaidia kuona mambo mengi, na kufanikisha mambo mengi pia. 

Si rahisi sana kuweza kufanikiwa sana kama akili yako haijatulia. Unatakiwa ujue, silaha yako kubwa ya mafanikio ni matumizi ya akili yako na wala si bahati au muujiza kama uwazavyo.

Akili yako ina uwezo wa kukupa matokeo makubwa sana kama imetulia, hapa inaweza ikakupa majibu mazuri na ikaleta matokeo ya kushangaza ambayo huwezi kuyaamini.

Hivyo, unatakiwa kila wakati kuchagua mazingira tulivu yatakayoifanya akili yako ifanye kazi kwa utulivu. Unatakiwa kuishi na watu sahihi, wasio na makelele kwako.

Lakini si hivyo tu, unatakiwa kuishi na mke au mume sahihi kwako asiye na makelele. Unatakiwa kuishi na mwenzi wako ambae anaifanya akili yako itulie na isiwe ya vurugu.

Amani ya akili, utulivu wa akili, ndio chanzo cha mafanikio makubwa yote na yakutisha. Hakuna ambae aliyefanikiwa huku akili yake ikiwa haijatulia, mtu huyo hayupo.

Waangalie vizuri watu waliofanikiwa, utajifunza kitu kimoja kwao ni watu ambao akili zao zimetulia. Unasema nimejuaje, angalia jinsi wanavyoongea, wanaongea kwa utulivu mkubwa sana, hiyo ni ishara akili zao zimetulia.

Ili kufukia mafanikio yako makubwa, haina haja na maana kuishi na watu au katika eneo ambalo linakunyima utulivu wa akili. Jiulize, ya nini kuishi na mpenzi ambaye anaifanya akili yako isitulie na kuanza kumwaza yeye. Tafuta utulivu wa akili utaona matokeo yake makubwa jinsi utakavyo yapata.

Unapokuwa na utulivu wa akili inakusaidia sana wewe kupangilia mambo na mikakati yako kwa ukamilifu, tofauti na ambavyo ukikosa utulivu akili yako haiwezi kuwaza kitu cha maana na kukupa matokeo makubwa. 

Zingatia sana, utulivu wa akili, ni silaha ya kwanza katika kufikia mafanikio yako. Kila siku, jitahidi, utafute eneo lilotulia na tafakari maisha yako, na utaona matokeo mazuri yakija kwa upande wako. 

Unatakiwa ujue, silaha kubwa katika kufikia mafanikio yako ni utulivu wa akili. Ukituliza akili zako, utafanya mambo makubwa sana na ya kushangaza wengi na pia wengi hawataamini je, kweli ni wewe. Kumbe siri, ipo kwenye kutuliza akili, basi.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.