google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 30, 2021

Njia Pekee Itakayokufanya Ukawa Hodari Ni Hii…

No comments :
Kuna watu ambao huwa wanatamani sana, wawe hodari katika jambo fulani. Watu hao hufika mahali hata kuwatamani watu ambao ni mahodari katika maisha yao na kujiuliza wamefikaje huko kwenye uhodari huo.
Nikwambie, ipo njia moja kubwa ya kukufanya ukawa hodari kwa kile unachokifanya, njia hiyo si nyingine bali ni kufanya kitu hicho kila siku bila kuacha. Kama utafanya jambo hilo kila siku na kwa njia tofauti za kujifunza basi utakuwa hodari.
Unapofanya jambo hilo kila siku, unatengeneza uhodari mkubwa sana ndani yako na mwisho wa siku unajikuta ni mshindi katika hilo eneo. Ukiwa unafanya jambo na kuliacha, huo uhodari utaupoteza tu.


Jiulize unataka kuwa hodari katika jambo lipi? Ukishapata jambo hili ambalo unataka kuwa hodari, anza utekelezaji wa kulifanya jambo hilo kila siku na kwa juhudi zote. Usijaribu kufanya na halafu ukaacha, hautaweza kuujenga uhodari kwa namna hiyo.
Watu wenye mafanikio, watu ambao unawaona wamefanikiwa, wamekazana kujenga uhodari kwa kuchagua kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu na si kugusa gusa na kuacha halafu ukategemea ukawa hodari.
Angalia maisha ya wanamichezo walio hodari ni kipi wanachokifanya, angalia maisha ya wajasiriamali wakubwa ni kipi wanafanya, utagundua ni watu ambao wameamua kuweka nguvu zao kwenye jambo moja kwa muda mrefu na kutengeneza uhodari.
Acha kuwa na ndoto za kukurupuka na kusema kwamba unataka kuwa hodari, unataka kufanikiwa sana na halafu kitu hicho unachotaka kukifanya hukifanyi kila siku. Kama haufanyi kila siku sahau mafanikio hayo unayoyataka.
Kama wewe ni mwimbaji, hebu imba kila siku. Kama wewe ni mwandishi, hebu andika kila siku, kama wewe mchoraji, chora kila siku na fanya hivyo kwa miaka kumi, na huku ukijifunza tuone kama hujawa hodari.
Ukiona vya elewa ujue vimeumbwa, hivyo ndivyo wahengfa walivyosema na hawakukosea hata kidogo. Na vivyo hivyo ukitaka uhodari, acha kujidanganya, kaza buti na fanya kila siku jambo lako litakupa mafanikio tu.
Hakuna uchawi wala muujiza kwenye kutafuta uhodari. Ule uhodari unaoutafuta kila wakati upo kwenye kufanya kila siku na tena ikiwezekana unaamua kufanya maisha yako yote pasipo hata kukwama mara moja, ukifanya hivyo nakwambia utafanikiwa.
Kumbuka, uhodari unakuja kwa wewe kuamua kufanya jambo unalolitaka kila siku. Amua leo kuutafuta uhodari wako mpaka watu washangae, kumbe siri kubwa ya uhodari huo inakuwa imejificha kwa wewe kuamua kufanya kila siku.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNERS, kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.