google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 29, 2016

Kama Unataka Kufanikiwa Ni lazima Uongozwe Na Jambo Hili Kwanza.

No comments :
Kisaikolojia kila binadamu anaongozwa na nafsi mbili ambazo ni hisia na Hoja .

Hisia ni hali ya utabiri isiyokuwa na uhakika wa jambo. Huenda ikawa na ukweli au uongo. Mara nyingi hisia hutawaliwa na tamaa ya macho au mwili. Hoja ni uhalisia wa jambo au mambo yanayoonekana kwa macho. Ni mambo yenye uhalisia kimtazamo. Mtu yeyote anayeongozwa na hoja hufanikiwa kwa 100% lakini mtu anayeongozwa na hisia au tamaa ni kama mcheza kamari, anaweza kupata au kuliwa au kushindwa kabisa.

Hisia kama tulivyoona ni tabia ya kimaumbile aliyonayo mtu. Kila mtu ana tamaa ya kupata mafanikio katika maisha yake. Hiyo ni hisia haina hoja ya msingi katika kuleta mafanikio. Mafanikio ili yapatikane lazima iwepo hoja ya msingi  itakayo tawala katika maneno na vitendo vya mtu katika maisha ya mtu. Kivipi kuwe na hoja za msingi?

Ukitaka mafanikio  lazima ujenge hoja za msingi na zenye mashiko. Ni lazima uwe tayari kuizishinda hisia za matamanio katika maisha. Uamue kuifanya akili yako iongozwe na hoja badala ya kuongozwa na hisia.

HOJA ZA MSINGI ZITAKUSAIDIA KUFANIKIWA.
Hoja humfanya mtu kuwa na uhakika wa kile anachokifanya. Kuwa na ‘data’ sahihi za kile anachofanya. Humfanya mtu kufanya kila kitu kwa ufanisi MKUBWA.

Hoja humfanya mtu kujiamini na kuthamini kile anachofanya. Hoja humpa heshima na kumfanya athaminike na jamii kutokana na kufanya vitu sahihi na vyenye tija kwa jamii. 

Hisia au tamaa humfanya mtu kufanya maamuzi yanayompelekea kujuta baadae katika maisha take.

Hisia zikimtawala mtu hufanya vitu vya aibu na kumdhalilisha katika jamii kama kuiba, kubaka, kulawiti, kusema uongo kwa manufaa binafsi, kula mali ya haramu bila Hofu. Hisia zikimtawala mtu hukosa kujiamini na kujiona mwenye mapungufu na kukosa ujasiri.

Katika kumalizia somo letu naomba kutoa angalizo kuwa kabla ya kufanya maamuzi katika jambo lolote unalohitaji kufanya kwanza jiulize unayotaka kufanya je, yanaongozwa na hisia au hoja? Kama yanaongozwa na hisia au tamaa kamwe usifanye jambo hilo na kama jambo hilo linaongozwa na hoja hakika lifanye maana litakufaa katika maisha yako.

Naomba tuishie hapa kwa leo tukutane muda ujao kwa ajili ya kujifunza zaidi na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kwa kina.

Tupo pamoja,

Shariff H. Kisuda (Mzee wa Nyundo)
Simu; 0715 079 993,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.