Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, August 9, 2016

Kinachowaathiri Wafanyabiashara Wengi Na Kufanya Biashara Hizo Kufa Ni Hiki.

No comments :
Siku zote kumbuka ya kwamba biashara ni mchakato, ninapozungumzia mchakato ni maana ya kwamba kuna kupanda na kushuka. Hapa nikiwa na maana ya kwamba kuanzisha biahara ni rahisi sana, ila endapo biashara hiyo ikifa kurudi tena katika kufanya biashara hiyo huwa ni vigumu sana.
Zipo baadhi ya sababu ambazo zinawafanya wafanyabiahara wengi wayumbe sana hasa katika biashara ambayo wanayofanya, najua wakati unaendele kusoma makala haya bado unashangaa ya kwamba nazungunza na nani?
Usishangae nazungumza na wewe, huenda ukawa unafanya biashara au haufanyi. Nazungumza na wewe ili uweze kuepukana na mambo ambayo yanafanya au yatafanya biashara yako ife.
Zifuatazo ndizo sababu ambazo zinawawathri wafanyabiashara wengi.
1. Kukosekana kwa elimu ya jinsi ya kukabiliana na ushindani katika soko.
Zipo biashara ambazo zinakuwa au ambazo tayari zimekwisha kua ambazo mara nyingi huwa zinateteleka kwa namna moja ama nyingine hasa linapokuja suala la ushindani wa bidhaa au huduma katika soko.
Wafanyabiashara walio wengi huwa wanakuwa na mtazamo mmoja tu. Mtazamo huwa ndio ambao unakuwa unawaathari kwa asilimia kubwa sana. Mtazamo huo huwa katika suala la mfanano wa utoaji wa huduma.
Kwa mfano unakuta bidhaa ambayo utanunua mahali fulani, ubora na wingi wa bidhaa vinafanana na mfanyabiashara/wafanyabiahara wengine. Kufanya hivi kunafanya kuwepo kwa kutoeleweka ni nani mmiliki au mwazilishi au huduma imenunuliwa kwa nani!

Hivyo ifike mahali kila mmoja wetu ambaye anafanya biashara kuwe na utofauti kati mfanyabiashara mmoja na mwingine, maana kufanya hivyo kutakutofautisha katika kutambulisha huduma au bidhaa kwa mteja.
Vilevile huna budi kuwa na utofauti na wengine kwa kuwa mbunifu katika biashara. Katika ulimwengu huu wa dunia ambayo inaenda kasi kuliko neno lenyewe huna budi kutumia teknolojia katika kujifunza kufanya biashara tofauti na watu wafanyavyo sasa.
Hata hivyo siri ya mafanikio ya kibiashara iliyojificha ni kwamba huna haja ya kuongeza mtaji mkubwa katika biashara ila inakupasa kuweza kuongeza thamani katika biadhaa au huduma.
Kwa  Mfano badala ya kuuza samaki ambao wateja wamezoea kwa shilingi elfu moja unaweza ukatumia teknolojia ya kuwakausha samaki, na kufunga katika vifungashio vizuri na kuuza samaki yule yule ambaye ulikuwa unamuuza kwa shilingi elfu moja na wewe ukaja ukamuuza kwa shilingi elfu tano.
Kufanya hivyo ndipo ninapozungumzia katika biashara yeyote ambayo unaifanya, fikiri kwa umakini sana na kwa jinsi gani unaweza ukaongeza thamani ya bidhaa au huduma kama ulivyoona kwa mfano wa biashara ya samaki hapo juu.
2. Kuwa na mtazamo hasi juu ya watu wanaokuzunguka kibiashara.
Biashara nyingi huwa hazikuwi au hufa kabisa hii ni kutokana na kuwa na mtazamo hasi juu ya mambo ambayo tunayafanya katika kibiashara. Watu wengi hususani watu ambao wanafanya biashara huwa ni ubinafsi sana.
Ubinafsi huu ndio ambao unazidi kujenga uhasama kwa asilimia kubwa hasa kwa wafanyabiashara wengine ambao wanakuzunguka. Ubinafsi huo ni kama ufutao.
Kwa mfano unaweza ukaenda sehemu fulani kununua bidhaa za jumla ila ghafla unakuta mtu huyo hana bidhaa fulani ila anajua kwamba jirani yake bidhaa hiyo anayo kutokana na ubinafsi wa kibiashara mfanyabiashira huyo hawezi kumuelekekeza mteja bidhaa hiyo atapata wapi? Zaidi ya kumwambia kaishiwa.
Au  mfanyabiashara huyo hawezi kwenda kumfuatia mteja bidhaa au huduma kwa jirani yake. Sasa kwa staili kama hiyo tutafanikiwa kweli? Hivyo wito wangu kwako ni kwamba ni lazima uwe na ushirikiano wa kutosha baina yako na wafanyabishara wengine ambao wanaokuzunguka.
Kufanya hivyo kutafanya kukuza biashara yako hasa katika ongezeko kubwa la wateja. Watu wengi hufanya hivi huku wakiamini ya kwamba kufanya hivi ni kuibiwa wateja wako  ila ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni kuongeza makuzi ya kibiashara na kuongeza wateja kwa ujumla.
“Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi” kwa kuendelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ndimi; benson chonya

0757909924

No comments :

Post a Comment