Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, August 10, 2016

Hii Ndiyo Dozi Sahihi Ya Maisha Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Mara kadhaa unatakuwa umekuwa shahidi kwa namna moja ama nyinyine kwa kuona ya kwamba mtu akiumwa ni lazima atafute matibabu ili aweze kupona ugonjwa  ambao unamsumbua.
Hivyo hivyo mtu huyo akipewa dawa  anatakiwa kuzitumia katika utaratibu ambao unaeleweka ili aweze kupona, utaratibu huo ndio ambao huitwa dozi, dozi hiyo lazima mtu aifuate ili aweze kupona na endapo atatumia kinyume  na alivyoelekezwa na mtalamu upo uwezakano mkubwa kuweza hudhurika zaidi au kupoteza maisha.
Kama ilivyo kwa mgonjwa ili aweze kupona na kuimarika vizuri katika afya yake hana budi  mgonjwa huyo kuweza kufuata utaratibu wa kutumia dozi ili aweze kupona.
Hata kwenye safari yako ya mafanikio ndivyo ilivyo, unahitaji kupata dozi, dozi ambayo ina misingi na utaratibu wake wa kuitumia. Wengi wetu tunamani kupata mafanikio kwa haraka zaidi, huku tukisahau ya kwamba mafanikio ni hatua kwa maana ya kwamba ni lazima tumalize dozi ndipo tupate mafanikio hayo.
Hivyo nakusihi uweze kufuatana nami ili uweze kujua namna ya kuweza kupata dozi ya mafanikio yako, pia suala si kupata dozi  tu, bali uzitumie katika maisha yako, na si kuzitumia tu bali  uzitumie ili upone ugonjwa wa dhiki,  shida na taabu za kimaisha ili uweze kupata mafanikio yako.
Vile vile nisisitize kwa kusema ya kwamba ili uweze kufika ambapo unataka ya kwenda kwa maana ya kupata mafanikio huna budi ya kuamini na kuwa mvumilivu na mbunifu wa hali ya juu  sana.
Ifuatayo ndiyo dozi sahihi ya safari yako ya mafanikio.
1. Angalia matumizi yako ya muda katika kutekeleza malengo yako.
Ipo haja leo ya kujua mambo ambayo yatakusaidia kuweza kutimiza malengo yako. Watu wengi huwa tunakosea sana hasa katika kujali na kuzingatia muda wa kutekeza mambo yetu.
Kwa mfano watu wengi licha ya kuwa na malengo huwa hatuweki ni kwa muda gani ndoto yako itakuwa imekamilika. Mfano ili uweze kufanikiwa na kutimiza malengo yako, kwa mfano unataka kuwa mfanyabiashara fulani ni lazima ujue ni muda gani  utakuwa umetiza jambo lako. Hii ni muhimu sana kuzingatia.

Hata hivyo kuwa na maono ya muda (time limit)kwa kila jambo lako itakusaidia kuweza kujua ni kwa namna gani utakuwa umetiza lengo lako.  Hivyo nakusihi kwa  kila jambo lako ambalo unatamani kulifanya kwa hapo baadae ni lazima uwe umelipanga  ni baada ya muda gani  lengo hilo litakuwa limekamilika. Pia mara kadhaa endelea kukumbuka msemo ule mtamu wenye kukutia hamasa ya kwamba ni ‘muda ni mali’ hivyo huna budi kulizingatia hilo.
2. Jifunze kutoka kwa watu walifanikiwa huku na wewe ukitumia njia ambazo ni za tofauti.
Mara kadhaa tumekuwa ni watu kulamika sana hasa pale ambapo tumefeli kwenye jambo fulani. Kulalamika huku mara kadhaa nimegundua ni kwa sababu kuu moja ya  kwamba tumejifunza kwa watu ambao wamefeli.
Lakini kufanya hivi mara kadhaa hutupa picha ya kwamba hata sisi hatuwezi hii ni kutokana mtu fulani alifeli. Kufeli kwa mtu  mwingine katika jambo lake kwa asilimia kadhaa hutengeneza hofu ndani yetu, hofu hiyo ni ile hofu ambayo utajiona ya kwamba hauwezi.
Hata hivyo kama unataka kupata mafanikio jambo la kuzingatia ni kwamba unatakiwa kupata ushauri kwa watu sahihi ambao wamekwisha fanikiwa kufanya hivi inakusaidia kwani wao wana taarifa sahihi kuhusiana na jambo hilo.
Kwa mfano unataka kufanya biashara ya kuuza chipsi ukiomba ushauri kwa mtu ambaye anauza mkaa, muuza mkaa huyo atakwambia biashara hiyo ina hasara sana, lakini sababu hizo sio za kweli kwa sababu hana taarifa sahihi, hivyo kama unataka kuuza chipsi ni lazima uweze kumfuata mtu ambaye amefanikiwa katika biashara hiyo kwani mtu huyo anazo taarifa kamili juu ya biashara hiyo.
Hivyo nakusihi ili uweze kupata mafanikio huna budi kuayazingatia hayo kwa hali ya juu sana, hasa katika suala la utekelezaji, kufanya hivyo kutukufanya uweze kuwa mshindi wa maisha yako. Endelea kufuatana nami katika safu hii kila wakati.
 “Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi” kwa kuendelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya


No comments :

Post a Comment