google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 4, 2016

Jinsi Muda wa Ziada Utakavyokutoa Kwenye Umaskini.

No comments :
Utafiti uliofanyika duniani umeonyesha Kuwa wengi wa wajasiriamali waliofanikiwa, walianza biashara zao kubwa kwa kutumia muda wao wa ziada. Ni mara Ngapi umesikia mtu akisema "ningependa kufanya biashara hii lakini tatizo sina muda?" 
Unapoona mtu akwambia sina muda maana yake ni nini? Ni kwamba huyo mtu hana motisha, nia wala shauku ya kufanya hicho Kitu ambacho umemshirikisha. 
kiuhalisia "Huwezi kukosa muda wa kufanya Kitu unachokipenda". Kwa Maana nyingine ni kwamba ukiona hujapata muda wa kufanya jambo fulani, basi ujue kuwa bado hujapenda au hujataka kufanya hivyo. 
Na wakati mwingine ni vizuri tukatambua kuwa kitu kinachoitwa muda ni Kitu kinachotengenezwa na sisi binadamu na kiuhalisia ni kwamba mara nyingi mpangilio wa shughuli zetu ndio unaotufanya ama tuwe na au muda tusiwe na muda kabisa. 
Kwa mfano, katika kila wiki kuna masaa 168. Je? Uliwahi kujiuliza masaa yote haya huwa yanakwenda Wapi? Hapa utaona kuwa matumizi ya masaa 168 ya wiki nzima yanatofautiana kulingana na mfumo wa maisha yako.
Katika ulimwengu huu, tunaweza Kusema kwamba kuna mifumo ya maisha aina mbili. Moja ni lile kundi la watu wengi wanaofuata maisha kwa kuuza muda na wapo watu wengine wachache wanaofuata maisha kwa kuwekeza muda wao. 
Maisha ya kuuza muda au "kubadilishana muda na pesa", ni maisha ambayo yanafuatwa zaidi na watu ambao ni waajiriwa pamoja na wale waliojajiri au kuajiriwa na biashara zao. Wewe kama ni muajiriwa, biashara yako kubwa ni kuwapa muda watu wengine halafu wao wanakupa pesa na maisha yanakwenda. 
Mgawanyo wa matumizi ya muda kwa wale wenye mfumo wa maisha ya kuuza muda kwa kawaida ni kama uko hivi: Katika wiki moja kuna masaa 168:
·                     Masaa 56 - Kulala
·                     Masaa 42 - Kula, kusafiri, muda na familia nk
·                     Masaa 40 - Kazi ya ajira
·                     Masaa 30 - muda wa ziada, Starehe na mengineyo.
Kwa kuangalia mgawanyo wa matumizi ya muda hapo juu ni kwamba, sisi wenyewe tunao uwezo wa kubadilisha matumizi ya muda uliopo. Kwa mfano: tunaweza sana kubadilisha matumizi ya masaa 30 Kwa wiki ambayo ni ya ziada na Starehe, yakawa ni masaa ya kufanya Kitu kwa ajili ya kutimiza ndoto yako au kukuletea utajiri siku za mbeleni.

Katika maisha tunaambiwa kuwa Kitu ambacho huwatofautisha matajiri na watu kawaida ambao ni katika matumizi ya muda. Watu masikini hutumia zaidi "muda wao wa ziada"  katika starehe kwenye. Wakati matajiri wao, hutumia sehemu kubwa ya muda wao wa ziada katika kujenga biashara zao. 
Hakika hali hii ndiyo imeleta mgawanyiko mkubwa na tofauti kubwa kimaisha kati ya walionacho na wasiokuwanacho.

Tafiti nyingi zilizowahi kufanyika duniani, zinaonyesha kuwa mtu wa kawaida anatumia zaidi ya masaa matano kwa siku kwenye starehe. Starehe tunazosema ni Kama vile kuangalia runinga, kuangalia mambo mbalimbali kwenye simu yako, filamu, kuangalia video za mbalimbali, vikao vya harusi na mengineyo mengi.

Lakini, hiyo haina maana kwamba usifurahie starehe yoyote, bali inabidi kufanya hivyo kwa wastani au kiasi. Kimsingi starehe hazitakiwi kula muda wako wa karibu moja ya tatu muda wako wa kufanya kazi kila Siku. Usifanye hivyo hata Kidogo.

Kila wakati ujiulize ni gharama kiasi gani unazilipa kutokana na tabia yako ya kuendekeza starehe? "Milion moja kwa mwaka? Milioni tano kwa mwaka? au kumi kwa mwaka? Au zaidi? Je utajisikiaje kama ukiachana na tabia ya kuendekeza starehe?.

Hapa tunaona Kuwa tunapata hasara mara mbili; Kwanza tunapoteza rasilimali muda na pili tunapoteza pesa.  Na je vitu hivi viwili tunavyovipoteza kila siku ndivyo vinahitajika sana katika kujenga mtaji wa kufanya mambo makubwa mazuri tunayoyatamani kila siku.
 Ukweli ni kwamba, kama unataka kutajirika, utatakiwa pengine kuanza biashara kwa muda wako wa ziada kuliko kusubiri sana. Huitajiki kuacha ajira au kazi yako ya ajira mara moja na pengine unaweza ukaamua kutokuacha ajira yako kabisa. 
Anza leo kujiambia Maneno haya kila Siku "sasa hivi nitafanya biashara kwenye muda wangu ziada hadi kufikia kwenye ndoto yangu”. Fikiria maisha yatakuwaje? Kwa hiyo inatosha kusema kuwa masaa 30 kila wiki yanapotea na wakati huo huo tunaendelea kuwa masikini na maisha kuishi ya kubangaiza kila siku. 
Lakini ni masaa hayo hayo 30 kwa wiki ambayo yakiokolewa na kuwekezwa vizuri yatakuweka huru na mwisho utakuwa mtu wa kusema "Biashara  yangu ilifanyika vizuri kiasi kwamba niliweza kuacha ajira". Wakati wa kuanza harakati za uokoaji wa masaa 30 yanayoangamia kila wiki ni leo
Endapo tukiacha masaa hayo yakaendelea kuangamia basi, tujue kuwa hatutabaki salama.
Imeandikwa na Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP BLOG

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.