google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 2, 2016

Tabia Za Pesa.

No comments :
Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini wengine wana pesa na kwa nini wengine hawana pesa? Kwa nini  wewe huna pesa ulikosea wapi au unakosea wapi? Ungana nami mzee wa Nyundo nikuhabarishe.

Kama ambavyo binadamu wana tabia zao zinazowaongoza na kuwafanya kuwa tofauti na wengine, pesa nayo ina tabia zake na kanuni zake pia. Pesa ina sheria zake  kuu nne:-                              

1. Namna ya kuitafuta na  kupatikana kwake.      

 2. Namna ya kuikuuza au kuifanya ikue na kuongezeka.    

 3. Namna ya kuilinda iendelee kuepo na kudumu.                        

 4.Namna ya kuitumia pesa.

Kisaikolojia kila binadamu awaye anajua namna ya kutafuta pesa na kutumia pesa. Ila tatizo na tofauti za hawa binadamu ziko katika tabia na namna zingine mbili kuikuza na kuilinda pesa na hapa ndipo hutokea tofauti kati ya wasionacho/masikini na walionacho/ matajiri.


 Daaah mzee wa nyundo leo umetoa kali. Kama umechungulia akili  za watu vile. Jamani  tuko pamoja au wengine nimewaacha njia panda ya Himo? Yes, wataalamu wa mambo ya maisha ya mwanadamu na mafanikio wamebaini katika tafiti zao kuwa KUNA UWEZEKANO WA KUPATA PESA KIRAHISI LAKINI NI NGUMU SANA KUPATA UTAJIRI KIRAHISI.

Why this? Tulia nikupe siri za mafanikio ya utajiri na mtu kupata pesa ni vitu viwili tofauti sana. Na hii ndio maana mtu anaweza kuzaliwa katika familia ya kitajiri na akawa masikini wakati kuna mtu mwingine kazaliwa familia ya kimaskini na leo hii ni Tajiri mkubwa sana.

Mfano kwa Tanzania ni Bakhresa na Mengi ni watu waliozaliwa katika familia duni lakini kwa kujua kwao na kuzifanyia kazi tabia za pesa. Leo wamekuwa ni watu wa tofauti na kuwa Matajiri. Hakuna njia ya mkato waliotumia kupata mafanikio waliyonayo.

Wamefuata sheria za pesa baada ya kujua tabia za fedha. Nawe unaweza kuwa Tajiri ukiamua kubadili matumizi yako ya pesa na kujua namna ya kuzifanya pesa zizae na kukua na pia kujua namna ya kuilinda pesa. Nitaikuzaje pesa na kuilinda Kisuda? Nawe unanichanganya akili yangu leo bro. Sikusomi kabisa. Daaah!!!

Kisaikolojia elimu zote hufundishwa darasani ispokuwa elimu ya pesa pekee  ndiyo haifundishwi darasani. Kivipi tena? Mzee wa Nyundo leo umeamua kunichosha kichwa changu. 

Elimu ya pesa hufundishwa pekee mtaani hata vyuo vinavyofundisha biashara na uchumi havifundishi hii Kitu. Ni mtaani pekee na kwa Kisuda mzee wa nyundo ndio mahali pekee unaweza kupata elimu hii muhimu na ya kipekee. Kivipi jibu rahisi, kesho amka asubuhi kisha mwendee tajiri mkubwa yeyote aliyeko mtaani kwako kamuuliza ni nini siri ya utajiri wake na mafanikio yake?

Hakika 100%  hakuna jibu la maana atakalokupa  zaidi ya kukuona kama mwanga na mchawi katika maisha yake. Kwa nini hii hutokea?  Hakuna anayetoa siri ya mafanikio yake ya kipesa kwa hofu ya kuzidiwa na wewe.

Siri wanazijua ila kukwambia wewe ni big no that's why Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kusaga rumba kila mwaka maisha ni yale yale no changes. Kila akijitahidi hapa na pale anaishia kubadilisha mboga na nguo za sikukuu na mwaka mpya.

Nihitimishe somo langu kwa kukupatia njia 5 za kuweza kufanya ili umiliki pesa na kuwa na uhuru wa kiuchumi au tajiri.                            

1.Weka AKIBA hii ni Kitu muhimu sana katika hatua za kukamata pesa. Weka Akiba angalau 10% kwa kila pato lako. Bila kujali ni kubwa au dogo kiasi gani tenga 10% kama AKIBA. Na kuna msemo moja huwa napenda kuutumia katika maisha yangu. Usiweke AKIBA kiasi kinachobakia baada ya matumizi Bali tumia kinachobakia Baada ya kuweka AKIBA yako ya 10%. Shika hii Mimi imemisaidia kufika malengo yangu mengi sana.                

2.Tafuta maarifa kwa kusoma vitabu na kuhudhuria semina na mafunzo ya watu sahihi na  wenye mawazo chanya.

3. Wekeza AKIBA yako katika miradi na biashara zinazolipa baada ya kupata maarifa na kujiridhisha vyakutosha.

4. Dhibiti matumizi yako ya Pesa kwa kuwa na Bajeti ya nini ununue na kwa nini ununue. tambua matumizi ya muhimu na matumizi yako ya lazima. Yape kipaumbele matumizi ya lazima kuliko matumizi ya muhimu hii nayo imenisaidia sana mmi Kisuda  kutimiza malengo na ndoto zangu Leo najivunia utambuzi huu katika matumizi kuhimu na ya lazima.

5. Kuwa na matumizi mazuri ya muda wako. Watu wengi hawana matumizi sahihi ya muda wao. Sio ni lazima uwe na ratiba itakayokuongoza katika siku yako. Kila binadamu ana masaa 24 lakini wachache hufanikiwa na wengi hawafanikiwi. Hapa kuna siri moja kubwa sana. ~Matumizi  sahihi ya masaa au muda wako wa  ziada ndiyo huamua eidha ufanikiwe au usifanikiwe. mzee wa nyundo umetisha sana Bro.

Siri ya wewe kuwa tajiri na kumiliki pesa zingatia vitu hivyo ni lazima ufanikiwe. Ukishindwa itabidi ukatambikiwe au ukaoge maji ya bahari.


Imeandikwa na mtaalamu wa masuala ya saikolojia na mafanikio SHARIFF KISUDA. Fuatan naye katika ukurasa wake wa face book, Shariff Kisuda ujifunze Siri za mafanikio  kila siku.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.