Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, August 15, 2016

Mambo Mawili Ya Kuzingatia Sana Ili Kufanikiwa

No comments :
Kitu kimojawapo kikubwa kinachotofautisha watu wanaofanikiwa na wale wanaoshindwa kwenye maisha ni MATENDO ama ACTION kama wenye lugha zao wanavyopenda kuita.

Haijalishi unajua nini, haijalishi unasema nini wala haijalishi una uelewa mkubwa kiasi gani! Hivyo vyote unavyojua na kusema, kama huchukui hatua ni sawa na kelele na havitaweza kukusaidia katika safari yako ya mafanikio.

Mafanikio ya kweli kwenye maisha yako siku zote yanakuja, ikiwa utajua kile unachotaka na kuchukua hatua za kuelekea kwenye mafanikio yako kila siku. Hapa ndipo mafanikio yako yanapoanzia.

Bila kuchukua hatua, halafu ukasema eti unatafuta mafanikio, hiyo itakuwa ni sawa na kujidanganya mwenyewe mchana kweupee.

Kitu cha kufanya na kukumbuka kila siku ikiwa unataka kufanikiwa na kujitofautisha na wale walioshindwa ni KUCHUKUA HATUA KILA SIKU, HATA KAMA NI KIDOGO bila kusahau kujua kile unachotaka.

Ukijua kile unachotaka na kuamua kuchukua hatua, hapo utakuwa upo kwenye njia sahihi ya kukamata mafanikio yako. Mambo mengine ya kukusaidia kufanikiwa kama kufanya kwa ubora, nidhamu binafsi au uvumilivu yatakuja yenyewe, lakini ikiwa utajua unachokitaka na kuchukua hatua.

Haya ni mambo mawili muhimu sana ambayo ukiyazingatia ni lazima ufanikiwe. Hata kama uliwahi kuitwa huwezi kufanikiwa tena, kilaza au eti una uwezo mdogo, Lakini ukizingatia kujua kile unachokitaka na kuchukua hatua, mafanikio ni yako.

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.

Nakutakia kila la kheri,

Imani Ngwangwalu.No comments :

Post a Comment