google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 30, 2016

Mambo Ambayo Watu Wenye Mafanikio Huyafanya Sana ‘Wikiendi’.

No comments :
Kimsingi, ipo tofauti kubwa sana kati ya watu waliofanikiwa na watu ambao hawajafanikiwa, husani katika suala zima la matumizi ya siku za mapumziko hasa wikiendi.
Mara nyingi watu waliofanikiwa huzitumia wikendi zao kwa manufaa zaidi ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa. Kutokana na matumizi haya ya muda huo wa mapumziko ndio wakati mwingine huweza kuleta utofauti hata wa mafanikio.
Hebu tuangalie watu wenye mafanikio huzitumiaje ‘wikiendi’ zao;-  
1. Kuamka asubuhi na mapema.
Mara nyingi watu wenye mafanikio, ratiba yao ya kuamka ipo pale pale bila kujali kwwamba ni siku ya kawaida au ‘wikiendi’. Siku zote hujitahidi sana kuweza kuamka asubuhi na mapema. 

Hufanya hivi kwa sababu wanatambua muda ni wathamani sana. Hivyo, hawako tayari kupoteza muda kwa chochote zaidi ya kuamka mapema na kuanza kuwekeza kwenye muda huo ili uwape faida.
2. Kujisomea.
Kati ya kitu amabacho watu wenye mafanikio huhakikisha wanakifanya wikiendi ni kujisomea. Kupitia kujisomea huko hujifunza mambo mengi ambayo yanawasaidia katika kukua kimafanikio na kupambana na changamoto za maisha.
3. Kutafakari juu ya maisha.
Watu wenye mafanikio katika wikiendi zao hawaishii kujisomea tu, bali wakati mwingine kutafakari sana juu ya maisha yao. Hutumia muda huo kujiuliza wapi walipotoka, wapi walipo na wapi wanapokwenda. Maswali hayo huwasidia kupiga hatua nyingine kubwa ya kusonga mbele.
4. Kufurahia maisha na familia.
Pia wikiendi kwa watu wenye mafanikio huzitumia sana kuwa pamoja na familia zao. Ni wakati ambao hupenda kucheza na kwenda maeneo tofauti na nyumbani kama ‘beach’ au mbuga za wanyama, kufurahia maisha na familia zao.
5. Kuweka mipango sawa ya wiki lijalo.
Mara nyingi watu wenye mafanikio huzitumia wikiendi zao, kwa kupanga mipango mipya ya wiki lijalo. Hapa hukaa chini na kujiuliza ni mikakati gani ambayo wataichukua ili kufanya wiki lijalo liwe bora na la manufaa zaidi.
6. Kufunga mawasiliano yasiyo ya muhimu.
Hiyo haitoshi watu wenye mafanikio ‘wikiendi’ zao huwa hawapendi sana kuwa na masiliano mengi kama ilivyo siku za kawaida. Kama ni simu wakati mwingine huzifunga au huwa hawapendi kuwasiliana sana na wengine katika kipidi hiki kifupi cha mapumziko.
7. Kutoa shukrani.
Shukrani ni jambo lingine la pekee ambalo watu wenye mafanikio hulifanya kwenye siku za mapumzikio. Ni kipindi ambacho huweza kuishukuru jamii kwa kwa namna tofauti mfano kutoa zawadi au kutembelea wagonjwa na mengineyo.
Kwa kifupi hayo ndiyo mambo machache ambayo watu wengi wenye mafanikio huyafanya sana katika siku zao za mapumziko ya wiki.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,

Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.