Dec 4, 2017
Mambo Ya Kuzingatia Unapokuwa Kazini Ili Usije Ukaishi Maisha Ya Majuto.
Wengi
wetu tunapokuwa makazini yapo maisha ambayo
tunakuwa tunaishi na yanapelekea majuto kwa baadae. Maisha haya wanayo
wengi sana, hasa vijana wanaopata kazi mapema na kujikuta kujuta baadae.
Unachopaswa
kujua au kuelewa, upo msingi wa maisha unatakiwa kuishi nao unapokuwa kazini
ili baade usije ukaishi maisha ya majuto na kujilaumu sana hasa pale unapofikia
uzeeni kwako.
Katika
makala haya itafafanua mambo ya kuzingatia unapokuwa kazini ili maisha yako ya
baade yawe ya uhakika na usije ukaishi maisha ya majuto. Sasa twende pamoja ili
tuweze kujfunza mambo hayo.
1. Tumia pesa zako kwa busara.
Kwa namna
yoyote ile unapokuwa kazini na unapata pesa zako wakati upo kazini, jitahidi
sana usiishi maisha ya kujisahau. Watu wengi wanapopata pesa wanakuwa
wanajisahau na kujua mshahara kwao ndio kila kitu.
Kwa mfano,
utakuta pesa unazipata kweli lakini matumizi yako yanakuwa yako hovyo sana,
kiasi kwamba unafika mahali huelewi hata hizo pesa zako unazitumiaje. Kuishi maisha
haya ni kutafuta janga kubwa la kushindwa kwa baadae.
Ili kuepuka
kuishi maisha ya majuto baade, ishi kwa mipango, pesa zako zipangilie vizuri na
ishi kwa kusudi maalumu.
2. Kamilisha mambo yako ya msingi
mapema.
Kama
unajielewa wewe upo kazini na umeamua kufanya kazi kweli, hebu kamilisha mambo
yako mapema. Yapo mambo ya msingi unayotakiwa kuyakamilisha mapema kama vile
kusomesha watoto na kujenga nyumba.
Ni kosa
kubwa sana, kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kujiandaa kujenga
nyumba yako na kusubiri hadi kustaafu kwako. Jenga nyumba mapema, maliza
kusomesha watoto wako mapema na usiache jukumu hilo kwa watoto wengine wakajisomesha
wao wenyewe.
Unapokamilisha
majukumu yako mapema inakupa uhuru wa
kuishi maisha bora pale unapokuwa umestaafu.
Kwa kifupi,
hayo ndiyo mamb unayopsw kuyazingatia has pale unapokuw kzaini na wakati huo
unajiandaa kutengeneza maisha bora uyatakayo.
Nakutakia
wakati mwema na uwe na siku njema, fanyia kazi haya na kila kheri katika
kufikia mafanikio yako.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.