google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 12, 2017

Siku Ya Kufanya Mabadiliko Makubwa Ya Maisha Yako Ni Hii…

No comments :
Ishi leo kama ndio siku maalumu hutakuja kuishi tena. Tumia muda wako wako vizuri, ongea na watu vizuri na tumia kila aina ya fursa uipatayo vyema na siku yako iwe na matokeo bora leo yatakayokusaidia baadae.
Kwa kadri unavyozidi kuishi leo yako kwa ubora, ndivyo ambavyo unazidi kubadilisha maisha yako na kuwa bora zaidi. Unasubiri nini kuishi leo kwa ule ubora wake unaotakiwa? Hutakiwi kusubiri kitu.
Kama leo una msongo wa mawazo, ule msongo wako wa mawazo uweke pembeni, akili zako na mawazo yako yote yaelekeze sasa. Kujilundikizia msongo ma mawazo wa nyuma na kuuleta sasa huko ni kutafuta kupoteza mengi katika maisha yako.

Leo ndio leo kwako ya kuweza kubadilisha maisha yako, leo ndio leo kwako ambayo unatakiwa uitumie kuweka juhudi kubwa sana bila kuzuiliwa na kitu. Hakuna wa kukushika shati kama ukiamua kuitumia leo kikomavu mpaka ukaweza kufanikiwa.
Washindi katika maisha wanaitumia leo yao vizuri. Hawana cha kusema kesho au ningejua, wanaweka juhudii leo na kuhakikisha kila kitu kinakamilka leo leo kwa wakati wake. Kwa nini sasa isiwe na kwako wewe?
Leo anza kutumia nidhamu yako vizuri, tumia muda wako vizuri na fanya kila ambacho ulitakiwa kukifanya kwa nidhamu ya hali juu hadi kifanikiwe, ukitumia nidhamu yako vizuri na ikawa endelevu, utafanikiwa.
Leo anza kutumia pesa zako vizuri ili pesa hizo zikusaidie wewe kuwekeza kwenye maisha yako kwa baadae na hatimaye kuweza kufikia uhuru wa kipesa. Usipoteze pesa zako hovyo kwa matumaini kwamba utazipata tena zingine.
Leo unaweza ukafanya chochote na lolote na baada ya muda utakuwa upo mbali sana kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,










No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.