Dec 23, 2017
MAMBO MUHIMU YAKUYAJUA KABLA YA KUINGIA KWENYE UFUGAJI.
Habari za leo rafiki, karibu sana katika kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusu ufugaji bora wa kuku, lengo kuu la makala haya kukupa elimu
iliyosahihi kuhusu ufugaji , Na mambo yote ninayoyaandika yanatoka kwenye
uzoefu wangu mwenyewe katika ufugaji karibu sana katika somo letu la leo.
Moja ya changamoto kubwa kwa watu wengi tunajiwekea malengo
makubwa kila mwaka kwamba nataka kufanya kile na kile ndani ya mwaka huu lakini
kila siku bado unashindwa kuanza hii inatokana na changamoto mbalimbali za hapa
na pale.
Pia wengi hushindwa kuanza kwa sababu kubwa ya kokosa hamasa ya ndani
juu ya kile walichokiwejiwekea malengo na hii inapelekea kila mwaka kuwa na
malengo yaleyale bila kupiga hatua na kwenye upande wa ufugaji mambo ni hayo
hayo kila siku.
Utakuta tunajisemea natamani kufuga huku tukiendea kuimba wimbo
usiokuwa na vitendo, nini ninachotaka kukwambia rafiki siku hii ya leo
unahitaji kuchukua hatua chukua hatua sasa nasiyo kusubili subili utachelewa
sana kufanikisha ndoto yako.
Unapochelewa kuchukua hatua ukumbuke siku zinaenda na majukumu
yanazidi kuongezeka huku umri nao unakimbia, ila rafiki yako nina jambo zuri ninalotaka
kukwambia na unatakiwa uchukue mara moja.
Jambo hili ambalo nakwambie uchukue hatua sasa ni juu ya wazo la
ufugaji. Unajua kwanini nakwambia ni sasa,
kwa sababu hakuna wakati mwingine mzuri wa kuanza zaidi ya sasa, anza kufanya na
kuweka mipango yako mapema juu ya ufugaji wako.
Hapa hapa nimekuandikia
mambo ambayo unatakiwa kuyajuwa kwanza na kuyafanyia kazi unapotaka kufanya
shughuli ya ufugaji za ufugaji ili uweze kufanikiwa katika ndoto yako ya
ufugaji, najua unafahamu kuwa ufugaji kwasasa ni moja ya kazi yenye faida.
1. ELIMU NA MAARIFA
SAHIHI KUHUSU UFUGAJI.
Hii imekuwa kama sehemu ya kujifichia kwa watu wengi
wanaposhindwa kuanza jambo lllote hasa la ufugaji unakuta wanaibuka na sababu
kuwa nashindwa kuanza kwasababu sina elimu sahihi juu ya ufugaji sasa sijui una
subiri nini kuitafuta hiyo elimu na maarifa sahihi unajichelewesha rafiki,
chukua hatua.
2. TAMBUA UNATAKA
KUFUGA KUKU KWA MALENGO GANI.
Nimuhimu kujua kwa nini unataka kufuga kuku kwa sababu ukijua
kwanini unataka kufuga kuku itakupa picha halisi juu ya kuku unaotaka kufuga
ili uweze kutafuta taarifa sahihi juu ya ufugaji wako kwasababu kuna aina
nyingi za kuku na kila kuku ana sifa zake na mahitaji yake hivyo ukijua malengo
yako kuhusu ufugaji wako itakusaidia sana katika kufanya maamuzi na kutafuta
taarifa sahihi kuhusu ufugaji wako.
3. ENEO UNALOTAKA KUFUGIA.
Unapojua tayari malengo uliyonayo katika ufugaji na kujua aina
ya kuku unaotaka kuwafuga sasa utakuwa na picha nzuri juu ya ufugaji wako,
baada ya hapo unahitaji kujuwa ENEO GANI UNALOTAKA KUFANYIA UFUGAJI hii
itakusaidia kujuwa mali ghafi ambayo itatumia katika banda lako, ni muhimu sana
kuandaa eneo la kufugia mapema mara tu ya kuweka malengo yako ya ufugaji, jua
eneo la kufugia mifugo yako.
4. GHARAMA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUFANYA UFUGAJI WAKO.
Baada yakujuwa malengo eneo unalotaka kufanyia shughuli zako za
ufugaji ni muhimu sana kuchanganua gharama zitakozotumika katika kuanza ufugaji
gharama hizo ni pamoja na banda, chakula, chanjo na tiba, hii itakusaidia
kuweka mipango yako sasa ili uweze kufanya ufugaji wako kwa ufanisi mzuri
5. ANZA NA ULICHONACHO.
Hii ni jambo la muhumu sana katika kutimiza malengo ya aina
yeyote, ni muhimu kuanza na kile ulichonacho usisubiri hadi uweze kujipanga
vizuri sana kwasababu unapoanza inakupa hamasa ya kuendelea kuchukua hatua
mbalimbali kuhusu ufugaji. Anza na kuku idadi yoyote, kama ni kumi, hamsini au
hata mia mbili kulingana na uwezo ulionao, kikubwa anza na ulichonacho.
Naomba niishie hapa kwa leo,
Endelea kunifatitia nina mengi mazuri yakukwambia kuhusu ufugaji
naamini yatakusaidia sana.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni Mimi rafiki yako katika ufugaji,
Frank Mapunda,
0758918243/0656918243
Karibu sana,
*
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.