Dec 11, 2017
Ili Kuepuka Makosa Ambayo Uliyoyafanya Mwaka Huu, Katika Mwaka Ujao Unatakiwa kuwa hivi:
Siku
ya leo nimejikuta nakumbuka sana enzi ambazo nilikuwa nasoma shule ya msingi,
nimekumbuka kwa sababu kila nikifanya mtihani nikumpa mzazi alikuwa haangilia
zile tiki ambazo nilikuwa nimepata bali alikuwa anaangalia maswali niliyokosa,
kisha alikuwa ananihoji mwanangu kwanini umekosa hizi, hapo ilikuwa haijalishi
nimepata alama kubwa kiasi gani? Mara baada ya kukosa majibu ni kwanini
nimefeli basi nilikuwa nakula mboko zangu za kutosha.
Kwa
kipindi kile niliona mzazi ananionea kwa
sababu binafsi nilijiona nimefaulu sana,
lakini kadri siku zinavyozidi kwenda nimekuja kutambua kumbe mzazi alivyokuwa
anafanya vile alikuwa sawa kabisa, unajua ni kwanini alikuwa sawa? Nakusihi
twende sawa mwanzo mpaka mwisho wa makala haya.
Ziliwa
zimebakia siku kadhaa kuamaliza mwaka huu, siku ya leo naomba ufanye tafakari
kwa kutazama malengo yako ambayo uliyapanga, angalia malengo hayo yamefikia
wapi, kwa sababu yawezekana kabisa ulikuwa umepanga kufanya jambo fulani na
mpaka dakika hii ukawa hujafikia lengo lako au umefanikiwa katika lengo hilo.
Endapo
kama umefikia lengo lako kwa asilimia zote piga kifua chako mara tatu huku
ukisema “asante Mungu kwa kunifanikisha jambo hili”.
Na
endapo kama hujafikia lengo lako ninachotaka kusema ni kwamba hizo ndizo alama
ambazo umekosa ambazo unatakiwa uzingalie, kuliko kuangalia zile alama ambazo
umezipata (malengo uliyoyatimiza).
Kuangalia
jambo ambalo hujalikamilisha, humfanya mtu atafakari ni wapi ambapo umekosea na
kuanza upya kulitekeleza, lakini jambo hili hufanywa na watu makini tu, bali
watu ambao sio makini wao hukata tamaa mapema na kujiona hawawezi tena.
Hivyo
kwa kuwa mwako ujao hutaki kufanya tena makosa, na pia kwa kuwa unataka kuona
unatekeleza jambo lako kwa wakati ambao umejipangia hivyo ni lazima uhakikishe
unafanya maamuzi magumu.
Nasema
ufanye maamuzi magumu kwa sababu, yeyote yule ambaye unamuona amefanikiwa
katika dunia hii ni kwamba ni lazima ipo siku moja mtu huyo alifanya maamuzi
magumu.
Msomaji
mwingine atanyoosha kidole na kusema
afisa mipango maamuzi magumu ni yapi?
Nami
bila hiana namwambia maamuzi magumu ni
yale ambayo yatafamfanya mtu asiwe wa kawaida hata vitu anavyofanya asifanye
kwa kawaida na alivyozoea kwani akifanya kwa kawaida na alivyozea basi hata matokea
ya jambo hilo litakuwa ni ya kawaida.
Lakini
pia kufanya maamuzi magumu ni lazima ujikane mwenyewe, kwa sababu mafanikio ni
gharama lakini pia ni lazima ukubali kuwapoteza marafiki ambao hawana msaada
wowote katika maisha yako.
Hayo
ni baadhi tu ya maamuzi magumu ambayo unatakiwa kuyachukua siku ya leo ili
uepuke makosa ambayo uliyafanya mwaka huu.
Na
mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba ili uweze kufika mbali zaidi katika
kutimiza malengo yako kwa mwako ujao hakikisha ya kwamba unafanya maamuzi
yasiyo ya kawaida.
Ndimi
afisa Mipango wa Mafanikio Benson Chonya,
0757-909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.