google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 13, 2017

Fanya Maisha Yako Yawe Bora Kwa Kujipa Changamoto Hii…

No comments :
Ipo njia au namna ya kuyapa maisha yako nguvu na ikakupelekea wewe kupambana na changamoto yoyote pasipo ya hofu. Njia hii si nyingine bali kuamua kujipa changamoto wewe mwenyewe na sio kuzisubiri.
Hakuna namna unavyoweza ukafanya maisha yako yakabadilika sana kama huna changamoto. Ukumbuke changamoto ninazozingumzia hapa ni  zile za kujiwekea yaani hapa wewe unaamua sasa najipa changamoto hii halafu unasikilizia matokeo.
Kwa mfano, unaona kabisa kipato chako imefika wakati unaona kidogo kwa kifupi,  hakitoshelezi. Hapa unaweza ukajipa changamoto na kusema sasa ndani ya miezi minne nitahakikisha naongeza kipato changu kikue kwa laki moja kila mwezi.

Pengine labda una mradi unaotaka kuuanzisha, na ambao pia unahitaji pesa, hapa pia unaweza ukajipa changamoto na kusema kila mwezi lazima nipate kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya mradi wangu huu.
Pia unaweza ukawa ni mwanariadha, kila wakati unakimbiakia kilomita kumi yaani hapo ndio mwisho wako. Unaweza ukajipa changamoto kwa kuongeza kilomita zingine tano za kukimbia wewe mwenyewe bila shuruti ya mtu.
Na kweli kutokana na changamoto hizo unazojiwekea utashangaa unatimiza malengo yako, ingawa mwanzo inaweza ikawa ni shida, lakini mwisho wa siku malengo yako yanatimia na kufika kule unakotaka kufika.
Kujipa changamoto kwa namna hiyo ni njia mojawapo ya kuweza kukua na kufanya wewe kuwa na uwezo wa kukabaliana na changamoto yoyote bila tabu. Hatua unayotakiwa kuanza nayo wewe  ni kujipa changamoto.
Hapa unachotakiwa kuangalia ni eneo lipi ambalo hufanyi vizuri, kisha jipe changamoto ya kuweza kuboresha eneo hilo. Huhitaji kujiwekea changamoto kubwa sana unaweka kidogo, ukiivuka, unaongeze tena.
Hivyo ndivyo unavyoweza kujipa changamoto na kuzishinda na hatimaye lakini utakuwa umetengeneza maisha unayotaka wewe yawe hivyo. Kitu cha kufanya kwako leo ni kutafuta wapi ambapo unakwama na kisha jipe changamoto zaidi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.