Dec 18, 2017
Bila Kujali Kitu Gani Kinatokea, Taka Matokeo.
Ugunduzi
mkubwa duniani, ulianza au ulitokana na watu ambao walikuwa wana matatizo sana.
Kwa mfano, kuna eneo fulani duniani ambapo watu walikuwa wakitembea kwa miguu,
kutokana na kuchoka huko kutembea kwa miguu ndio utakaja ugunduzi wa magari na
hata ndege ili kurahisha.
Ubunifu
mkubwa duniani pia ulitokana na watu ambao walikuwa hawajaridhishwa na huduma
zinazotolewa. Kwa mfano, watu baada ya kuchoshwa na mabasi yenye ‘keria’ juu hapo ndipo yakaja mabasi yenye
‘buti’ ili kuepusha hata upotevu wa
mizigo na inakuwa salama wakati wote.
Mafanikio
makubwa duniani pia yanazaliwa na watu ambao walikutana na changamoto nyingi
sana. Kuna watu baada ya kuchoshwa na umaskini, basi waliamua kupigana usiku na
mchana mpaka kuhakikisha wanaupa umaskini mkono wa kwaheri, hakuna umaskini uliotolewa
kwa njia ya lelemama.
Hii
yote inadhihirisha kuwa, mafanikio makubwa hayaendi kwa watu ambao wanasema
siku nikipata muda au siku nikipata pesa za kutosha basi nitawekeza kwenye
mradi wa aina fulani, bali mafanikio makubwa yanaenda kwa watu wote ambao wako
tayari kuchukua hatua hata kama rasilimali zao kwa akili na macho zinaonekana
ni kidogo sana.
Hebu
jiulize aliyegundua ndege au aliyegundua meli ni pesa au rasilimali gani za
kutosha alikuwa nazo? Ukiangalia elimu, hawakuwa nazo za kutosha, ukiangalia ni
pesa hawakunazo za kutosha, kila kitu kilikuwa hakitoshi kwao, lakini
kilichowasukuma ni kutaka matokeo wanayoyataka bila kujali wana rasililmali
chache kiasi gani.
Lakini
tunaona mwisho wa siku, kutokana na ung’ang’anizi wao huo wakaja na kitu
kikubwa, endapo kama wangekaa na kuanza kulia lia kama wewe unavyolia kwamba ‘ooh sina mtaji na siwezi kufanya biashara,’
basi inawezekana kabisa leo hii tungekuwa labda tunatembea kwa miguu.
Maisha
ya mafanikio yanataka utayari. Upo tayari kutoa nini? Kwa chochote kile ulichonacho
mkononi mwako hata kiwe kidogo sana kina uwezo wa kukufanikisha ikiwa kitu
hicho utakilea na kukitunza vizuri. Haijalishi iwe ni kazi ya mshahara kidogo
au una biashara ndogo lakini unaweza kupiga hatua na kufika mbali sana
kimafanikio.
Kwa
nini uendelee kuteseka na kuamini kwamba huwezi kufanikiwa, wakati uwezo huo
unao. Kipi kinachokurudisha nyuma, je umeamua kukwama kwa sababu unaamini
kwamba wewe si kitu na hutaweza kipiga hatua kwa sababu ya rasilimali ulizonazo
ni chache sana, hiyo tu ni kwambie si kweli hata kidogo.
Kuanzia
leo, acha kabisa kusubiri kuwa kamili, fanya kila ufanyalo kuhakikisha unapata
matokeo unayoyataka. Kama unataka kwekeza kwenye mradi wa aina fulani, wekeza
pasipo kutafuta sababu yoyote ile. Sababu hazina nafasi kwenye mafanikio yako,
unatakiwa kufanikiwa tu.
Vizuizi
au vikwazo vipo tu katika maisha yako. ukitafuta sababu kwamba ipo siku
utavikimbia vizuizi hivyo hapo utakuwa unajidanganya sana. Tafuta njia ya
kuweza kuondokana na vizuizi hivo ili uweze kuwa mshindi wa maisha yako. Kwa namna yoyote ile, bila kujali nini
kitatokea, taka matokeo ya mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.