Dec 17, 2017
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Hakuna Mkate, Pasipo Kazi.
Naamini
leo yako iko poa na unaendelea kuimalizia wikiendi yako kabla ya kesho hujatua
kazini kuanza kukamilisha majukumu ya Juma zima. Kama iko hivyo, shukrani za
pekee zimwendee Mola wetu.
Ni wakati
na jumapili njema kabisa nami na kualika katika jamvi letu la Hekima za maisha
na mafanikio. Kumbuka hizi ni hekima ambazo zilitolewa kitambo na babu zetu au
wahenga, sasa pia nasi ni muhimu tujifunze.
Na
kwa nini tunajifunza misemo au maneno ya wahenga wetu ni kwa sababu, wengi wetu
enzi hizo kwanza hatukuwepo, kwa hiyo kwa kujifunza hapa kupitia ukurasa huu, vipo
vitu vizuri vya maisha na kimafanikio ambavyo vitatusaidia sote kutujenga kifikra
na kimaisha.
Kwa
kuwa na mimi si mchoyo, na sipendi kukunyima kitu, naomba nikukaribishe moja
kwa moja na twende tujifunze hekima na mafanikio ambazo nimekuandalia siku ya
leo. Kikubwa kaa mkao wa darasa na karibu sana.
Hekima ya 1; Hakuna mkate, pasipo kazi.
Hekima
hii inajipambanua na iko wazi ikiwa na maana kwamba pasipo kazi, usitegemee
mafanikio. Kama utakuwa umekaa tu na huweki juhudi za makusudi za kukusaidia
kuweza kupata mafanikio yako, sahau kuhusu mafanikio. Mafanikio yanakuja kwa
kazi, na kazi ndio inatupatia mkate au ridhiki ya kila siku.
Hata
vitabu vya dini vimeweza kuandika hili ‘asiyefanya
kazi na asile’ na hicho ndicho kitu unachopaswa kuzingatia. Kama unataka
mavuno ya aina fulani, jiulize ni kazi ipi ambayo umeifanya. Kumbuka wahenga wetu
kutokana na hekima zao wanasema wazi,
hakuna mkate, pasipo kazi na hio ndio kweli halisi huwezi kupinga.
Hekima ya 2; Unapokwenda kununua kitu,
tumia macho na usitumie masikio tu.
Ni mara
nyingi sana wengi wetu tunapokwenda kununua vitu iwe dukani au sokoni, huwa
tuna tabia ya kuwasikiliza sana wale wanaotuuzia na kusahau kabisa kuangalia
ubora wa kitu. Matokeo yake sasa, tunajikuta ni watu wa kuingia hasara kwa
kuchukua vitu vibovu. Utakuta mtu anasikiliza sana maelezo bila hata na yeye kuangalia
ukweli uko wapi.
Tabia
hii wanayo wengi sana, miongoni mwao inaweza ikawa ni hata wewe, lakini hapa
leo hekima hii inatukumbusha hivi, unapokwenda kununua kitu, tumia macho pia na
usitumie masikio peke yake. Hiyo ikiwa inaonyesha kwamba ni vyema kujiridhisha
kwa macho yako na si kusikiliza peke yako. Kusikiliza peke yake ni sawa na
kuamua kuingia hasara.
Hekima ya 3; Ushauri mzuri, ni bora kuliko dhahabu.
Hii ni
hekima ambayo msingi wake umejikita
katika kuonyesha kwamba ushauri mzuri siku zote ni bora kuliko dhahabu. Unaweza
ukapata dhahabu leo au mafanikio makubwa leo, lakini kama huna ushauri mzuri hiyo
ni sawa na bure, kwani ni rahisi hata kuweza kuipoteza hiyo dhahabu au kitu cha
thamani ulichokipata kama huna ushauri wa maana.
Kwa hiyo
hapa tunaonywa kuwa ni bora kupata ushauri mzuri kwanza, na kisha ushauri huo
mzuri utakusaidia kuweza kutumika katika kupata mafanikio makubwa ambayo
yanafananishwa na dhahabu. Mifano hai tunayo, waangalie watu wote ambao
walipata ushauri mbovu na maisha yao pia yapo hovyo pia.
Hekima ya 4; Usijilinde sana kwa kutumia
fensi, jilinde kwa kutumia marafiki.
Wapo
watu ambao katika maisha wanaamua kujilinda sana kwa kutumia kuta za nyumba,
wanajilinda sana kwa kutumia fensi na vitu vingine kama hivyo, na kusahau kuwa
kujilinda huko kunaweza kukawa kwa bure kama usipojua kwamba hata marafiki
ulionao pia nao ni walinzi wazuri tu.
Katika
hekima hii inatuonyesha kwamba ulinzi mzuri na wa maana upo kwa marafiki zetu
pia. Marafiki zetu ndio watakaotuambia kipi kizuri na kipi kibaya. Pia marafiki
zetu ni rahisi wao kutuonyesha marafiki wengine
wabaya na wepi ni wazuri. Kupitia hekima hii ya maisha na mafanikio ni wajibu
wetu kutafuta marafiki bora ili wawe walinzi kwetu.
Naamini
mpaka hapo kutokana na hekima ulizojifunza kuna kitu cha kipekee ambacho
umejifunza. Nikutakie wakati mwema na tukutane wiki ijayo kwa hekima zingine
kama hizi za maisha na mafanikio. Kila la kheri.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.