Apr 27, 2015
Kama Unataka Mafanikio Makubwa, Hakikisha Unabadili Kitu Hiki Haraka Sana.
Habari za leo mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO, nimatumaini yangu ya kuwa umzima na unaendelea vyema katika shughuli nzima ya kuboresha maisha yako. Kama nilivyosema katika makala iliyopita kuwa katika makala ya leo tutajifunza juu ya kubadili fikra zetu ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Ikumbukwe kuwa fikra ni kitu
cha muhimu sana kutuwezesha kufikia mafanikio makubwa tuliyojiwekea. Bila kuwa
na fikra sahihi ni vigumu sana kuweza kufikia mafanikio yoyote yale. Hivyo, hiyo
inatuhakikishia kuwa kama kweli unataka mafanikio makubwa, kitu cha kwanza
unachotakiwa kukibadili kwa haraka ni fikra zako.
Kumbuka,kufikiri ni
kufikiri, wengi ndivyo tunavyamini. Huwa tunachukulia kufikiri kwetu kama jambo
ambalo halituhusu kabisa. Inawezekana kabisa hapo ulipo ulishasahau kwamba huwa
unafikiri hadi hivi sasa unaposoma
kuhusu kufikiri.
Ni ajabu sana kwa sababu, huku
kufikiri ndiko kunakokufanya tuhisi au kutenda kwa namna hii au ile maishani.
Kila tunachofanya na mengi kama siyo yote kati ya yale yanayotutokea kwenye
maisha yetu yanatokana na kufikiri kwetu.
Katika kutafuta kufanikiwa
ni lazima kufikiri kwetu kuwe katika mkabala wa kufanikiwa kwanza. Kama
kufikiri kwetu kuko katika mkabala wa kushindwa, tunakuwa sawa na mtu anayeomba
watu wasukume gari lake kwenda mbele huku akiwa tayari amewaomba wengine
kulisukuma gari hilo kurudi nyuma.
Kama binadamu,
tunatofautiana katika mambo yanayoenda vichwani mwetu na mambo hayo ni mengi
sana. Wataalamu wamethibitisha kwamba, kwa kutwa moja binadamu anapitiwa na
mawazo zaidi ya elfu hamsini. Lakini jambo ambalo hatutofautiani ni ukweli
kwamba, kufikiri kwetu huko kwa namna-kufikiri kuzuri na kufikiri kubaya.
Singependa kuzungumzia
kufikiri vizuri na kufikiri vibaya kwa sababu, inahitaji maelezo mengi na hata
hivyo, haitasaidia sana katika muktadha huu. Bali ninachoweza kusema ni kwamba,
kufikiri vizuri ni ile hali ya kuingiza fikani mwetu yale mambo ambayo
hayatuumizi kihisia, kiroho na kimwili, wala kuwaumiza wengine kwa njia hiyo.
Kufikiri vizuri ni kuingiza
fikirani mwetu yale tu ambayo tunaamini kwamba yatatupa moyo, kutuongezea
matumaini na kutujengea uhusiano mzuri na wengine. Yale tu ambayo ndiyo
tunayotaka , tunayoyatamani na kupenda yatokee maishani mwetu.
Kufikiri vibaya, kwa kifupi
naweza kusema kuwa ni kufanya kinyume na kufikiri vizuri. Pale ambapo kile
tunachokiruhusu kuingia fikrani mwetu ni chenye kutuumiza kihisia, kiroho na
kimwili au kuwaumiza wenzetu kwa njia hiyohiyo, ndipo tunapaswa kujua kwamba,
tunafikiri vibaya. Kufikiri vibaya ni kuingiza mawazoni mwetu yale tusiyoyataka
au kuyatamani ama kuyapenda.
Unachopaswa kufanya kama
kweli unataka mafanikio maishani mwako ni kujiuliza kuhusu mfumo wako wa
kufikiri . je, mawazo yako mara nyingi yanabeba mambo gani?
Inawezekana kabisa huwa
unaamini kwamba wewe ni dhaifu, wewe huwezi kupata cheo, wewe huwezi biashara
fulani kama wengine au wewe ni msindikizaji tu. Kama unajiita ‘mlalahoi’
hujitendei haki. Kama unajiita ‘dhaifu’hujitendei haki. Kama unajiita mnyonge
hujitendei haki. Kama unajiambia una mkosi ndiyo kabisa na kama unajilaumu kila
wakati, tambua kwamba unajifuja kupita kiasi.
Kama unafikiri vibaya
inabidi ubadilike na kuanza kufikiri vizuri, yaani kuingiza fikrani mwako yale
tu ambayo yatakusaidia katika kufika kule unakotaka bila kujiumiza au kuwaumiza
wengine. Kuingiza ffikrani mwako yale tu unayotaka au kuyatamani, na siyo kuingiza yale
usiyoyataka.
Kwamba unaweza kufanya au
kupata kile unachokitaka maishani ni jambo lililowazi kabisa, bila kujali kama
umesoma au hukusoma, un rangi nyeusi au nyeupe, unatoka kwenye familia maskini
au ya kitajiri, unasali au husali. Sifa au vigezo vya kupata kile unachokitaka
vinafahamika, lakini kama nilivyosema sifa ya kwanza ni kufikiri.
Wale wote waliofanikiwa,
ukiwauliza watakwambia kwamba waliamini kuwa watafanikiwa walifanya juhudi
wakijua kuwa iko siku. Kuna wakati rais wa zamani wa marekani Abraham Lincolin(
Alikuwa rais mwaka 1860) ambaye alianguka na kushindwa zaidi ya mara ishirini
katika mambo mbalimbali ikiwemo katika uchaguzi, kufilisika biashara na hadi
kuchaganyikiwa. Lakini aliendelea bila kusema , ‘ninamkosi’ au ‘siwezi’ hadi
akaja kuwa kiongozi maarufu duniani.
Kwenye kitabu chake cha Unlimited power, Anthony Robbins
anamzungumzia mtu ambaye alipata ajali ya barabarani akaumia sana kiasi ch
akuharibika kabisa mwili. Mtu huyu alikuja tena akapata ajali yaa ngege ambapo
alipooza kuanzia kiunoni kwenda chini. Bila kujali ulemevu na uharibifu wa sura
na mwili, mtu huyu alisema, ‘ninawea na nitafanya’. Aliweza na kuwa miongoni
mwa mamilionea wa marekani. Kwa wenzetu wengi, kwa ulemavu wa aina hiyo
hunyoosha miguu na kuanza kuomba wakiamini hawawezi tena.
Anthony Robbins mwenyewe
hakusoma zaidi ya elimu ya kidato cha sita, lakini kwa kuamini kwamba,
inawezekana mtu anapoamua, alifanya maajabu. Kwa kiwango chake hicho cha elimu
aliweza kwa muda mfupi tu, kutoka katika hali ya uhohehahe wa kuishi chumba
kimoja chenye mende, hadi kuaminika katika kuwafundisha watu kuhusu maisha
wakiwemo viongozi wan Nchi.
Sasa hivi Robbins ni
bilionea na hakuiba wala kutumia
ujanjaujanja, bali kanuni za kimaumbile katika kujenga uwezo wa binadamu. Kama
angeamini kuwa, kwa sababu hakusoma sana asingeweza, ni wazi asingeweza, lakini
wa sababu hakujiwekea vizingiti amemudu.
Uwezo wa mawazo yetu
unaonekana vizuri kwa mtu na wazi kwa zaidi kwa mtu aitwaye Stephen Hawking,
ambaye ni miongoni mwa wanasayansi bora ambao karne iliyopita na karne hii zimeweza
kumshuhudia. Kwa nini mtu huyu ni mfano bora wa namna mawazo yalivyo na nguvu?
Akiwa na umri wa miaka 13
aliugua maradhi yanayofahamika kama amyotrophic
lateral screrosis u lo gehrig’s, hali ambayo hulemaza mwili. Hawking alilemaa
mwili mzima isipokuwa shingo, kichwa na mkono wake wa kushoto. Pia alikuwa hana
uwezo wa kuzungumza.
Akiwa kwenye hali hiyo,
aliweza kufanya maajabu kwenye eneo la fizikia na kutoa nadharia nyingi ambazo
zimesaidia kuibadili dunia katika maeneo mbalimbali. Kwa kuamini kwamba
anaweza, kupania na kujua anataka nini, ameshangaza wengi. Kwa sababu bado yu
hai, atashangaza wengi zaidi.
Ukiweza kuyabadili mawazo
yako, yanauwezo wa kukupa mafanikio makubwa ukiamua. Kitu unachotakiwa ni
kuacha kabisa kujidharau na kujishusha, utafanikiwa.
TUPO PAMOJA KATIKA SAFARI YAKO YA
MAFANIKIO,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.