Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, December 26, 2016

Je, Unashindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Ya Changamoto? Fanya Hivi…

No comments :
Ni hali ambayo hutokea kwa wengi unapokutana na changamoto au tatizo fulani kuona kwamba kila kitu ni kibaya katika maisha, ingawa ukweli hauko hivyo.
Kwa sababu ya tatizo linalokakubali ni rahisi kuona ndugu, rafiki, jamaa zako wote wa karibu ni wabaya kwa sababu huoni ule msaada wao wa moja kwa moja kukusaidia.
Usichokijua yote hayo yanapotokea si uhalisia wa maisha jinsi ulivyo. Hakuna mtu mbaya sana katika maisha yako hata mmoja. Si dunia wala ndugu zako ndio wabaya sana, vitu vyote hivyo viko sawa.
Mbaya wa kwanza katika hayo yote unayoyaona ni wewe mwenyewe, inawezekana hukusaidiwa kwa sababu ni kweli watu hao hawakuwa na uwezo. Sasa kwa nini ulalamike.
Kama hali au tatizo uliloingia limesababishwa na mwingine kwa namna moja au nyingine, jiulize wewe unamchango gani wa kusababisha hali hiyo kutokea? Kwa sababu ni lazima uwe na mchango wa aina fulani.

Hivyo unapoona una changamoto, ama tatizo fulani badala ya kulalalimikia wengine au kuumia  chukua hatua muhimu ya kuweza kutatua tatizo hilo mpaka uweze kulishinda.
Kujijengea tabia ya kuwa na lawama sana hakuwezi kukusaidia kitu hata siku moja. Unajiona una tatizo au changamoto likabili kwa nguvu zote bil kutafuta ‘mchawi’ wa tatizo lako.
Fanya kitu juu ya changamoto yako. Hakuna wa kukusaidia usipokubali kufanya kitu cha kuweza kukutoa kwenye changamoto ambayo inaweza ikawa inakukabili.
Unaweza ukawa ni kweli hujisikii vizuri, unajisikia vibaya sana kiasi cha kwamba unashindwa kuchukua hatua, lakini hebu fanya kitu ambacho kitakusaidia kutatua changamoto yako hata kwa sehemu kidogo.
Acha kuruhusu kusimama kimaisha kwa sababu ya changamoto zinazokuzunguka.
Acha kuwa chanzo cha kujiangusha mwenyewe kwa sababu ya changamoto za kimaisha.
Fanya kitu muhimu cha kukusaidia kuweza kusogea mbele kimafanikio hata ukiwa katikati cha matatizo au changamoto zinazokuzunguka.
Kutokufanya kitu, lisiwe moja ya suluhisho ambalo unaweza ukawa umechangua.
Kumbuka unao uwezo wa kubadilisha maisha yako ukiamua, changamoto zisiwe kizuizi kikubwa sana cha kukufanya ushindwe kufanikiwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com  

No comments :

Post a Comment