Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, December 30, 2016

Mabadiliko Katika Maisha Yako Hayasubiri Kitu Hiki...

No comments :
Upo uwezekano mkubwa sana kwa wewe kuamini kwamba kila mwaka unaanza utakuwa ni bora zaidi kuliko mwaka uliopita.
Upo uwezekano wa wewe kuamini sana kwamba kesho yako itakuwa ni bora sana kuliko ilivyo leo.
Pia upo uwezekano wa wewe kutokuchukua hatua  ndogo ndogo katika maisha yako na kusubiri kuchukua hatua hizo katika mwaka unaokuja.
Mipango na matumaini unayojipa naweza kusema ipo sawa kwa kiasi fulani, lakini tena wakati huo naweza nikakwambia haiko sawa kabisa. Ki vipi?
Badala ya kujipa matumaini nitafanya hili mwaka kesho au siku fulani na kuamua kutulia, hebu amua kuchukua hatua leo hii za kufanya kitu, hata kama ni kidogo.

Acha kusubiri mwaka mpya uanze, fanya mabadiliko ya maisha yako sasa.
Acha kusubiri hadi mwisho wa mwaka ndio uanze kutafakari kipi cha kuboresha na kipi sio cha kuboresha katika maisha yako. Jenga utaratibu wa kujikagua karibu kila siku na kuboresha maisha yako.
Tatizo kubwa ulilnalo unajipa muda sana wa kuahirisha mambo mengi ikiwa pamoja na mipango yako. Maisha tuliyonayo hayatusubiri hata kidogo. Kipo kitu ambacho unatakiwa kufanya kila siku ili  kufanya mabadiliko na kuboresha maisha yako.
Inawezekana ili kufanya mabadiliko ya maisha yako kuna maarifa unatakiwa uyapate. Pia inawezekana ili kufanya mabadiliko ya maisha yako kuna watu unatakiwa kushirikiana nao vizuri ili wa kusaidie kufikia ndoto zako.
Sasa kama iko hivyo ni kwa nini uendelee kusubiri hadi mwaka ujao?
Chukua muda mchache kila siku asubuhi kujiuliza ni kipi ambacho utakwenda kufanya ili kuboresha maisha yako?

Chagua jambo moja dogo tu la kufanya litakalokusaidia kuboresha maisha yako. Nimesema jambo moja tu, usichague mambo mawili au matatu, nimesema chagua jambo moja tu, ambalo unaamini litakuletea mabadiliko.
Hiyo yote inaonyesha mabadiliko ya maisha yako unaweza ukayaanza sasa na si kesho au wakati mwingine unaona ni bora zaidi kwako.
Mabadiliko katika maisha yako hayasubiri mwaka mpya uanze, mabadiliko yako hayasubiri kesho, unatakiwa kufanya mabadiliko sasa, kwani huu ndio wakati bora sana kwako.
Katika maisha, hakuna mtu ambaye ni rafiki wa kesho. Huwezi kujua kesho hiyo unayoisubiri ni nini kitatokea. Anza kufanya mabadiliko ya maisha yako sasa na si kesho au siku nyingine.
Ukichukua hatua hiyo utayapa maisha yako nguvu sana ya kusonga mbele kuliko ambavyo ungesubiri. Chukua hatua sasa. Ni muda wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
Tafakari juu ya hilo, chukua hatua na endelea kubadili maisha yako kwa kupata maarifa sahihi kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment