google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Dec 19, 2016

Je, Wajua! Kila Kitu Hutokea Kwa Sababu Maalumu?

No comments :
Kijana mmoja baaada ya kuhitimu masomo yake ya chuo alipanga kwenda kumtembelea mjomba wake ambaye kwa wakati huo alikuwa anaishi kijijini. Kijana Aliamua kufanya hivyo  kwani zilikuwa zimepita siku nyingi bila kuonana kwa mjomba wake.

Hivyo siku uliyofuata kijana aliamka asubuhi na  mapema kabla jua halijaleta faraja kwa watu wake, alijiaanda kwa  kasi zaidi ya 4G   kabla ya kuanza safari ya kuelekea kijijini kwani muda haukuwa rafiki kwake.

Kwa kuwa safari ilikuwa ni ndefu sana kijana huyo aliamua kubeba chakula ambacho kingemsaidia kupungunguza njaa wakati wa safari, safari iliendelea huku kijana mawazo ya mjini akiyaacha na wenye miji yao huku akili yake ikiwa ina shuaku na msukumo thabiti kuhusu maisha ya kule kijinini. 

Ilipofika mida ya muda wa mchana kwa kuwa njaa ilikuwa inamuuma sana alichua chakula chake na kuanza kula.


Aliuamini ule usemi ambao unasema "usiudharau mkono kwa sababu ya kijiko" hivyo chakula kile alikula kwa kutumia mkono ambao anaumini zaidi, lakini kama ujuavyo wakati wa safari utaratibu wa kunawa mikono wakati wa safari huwa si zingatio sana aliamua kula bila hata kunawa mikono yake.

Baada ya dakika chache kula chakula kile, tumbo la ghafla lilimkamata huku akikaa kila aina ya mkao ujuao wewe katika siti ile, alifanya vile ili kuyanusuru maumivu ambayo yalikuwa yametawala katika tumbo. Hata hivyo kadri muda ulivyozidi kuyoyoma na tumbo nalo lilikuwa linazidi kuuma zaidi.

Aliwaza ni kitu gani ambacho kimesababisha tumbo lake kuuma, lakini kadri anavyozidi kuzama katika dibwi la halmashauri ya fikra zake aligundua ya kwamba chakula alichokula kulikuwa ni  chanzo cha kuuma kwa tumbo lake.

Hivyo safari iliendelea mpaka alipowasili katika kijiji ambacho alikuwa anaishi mjomba wake.

Mjomba alifurahi kumuona kijana yule, lakini mjomba alishtuka kumuona kijana yule akiwa hana furaha, ndipo mjomba akaamua kushirikisha mdomo katika kumuuliza swali kijana yule ni kipi ambacho kimemtoa katika ulimwengu furaha, ndipo kijana akamueleza mjomba wake tumbo lilikuwa linamsumbua kidogo.

Baada ya mjomba kusikia hayo alimueleza ya kwamba asipate tabu kwani atakuwa sawa muda si mrefu, walipofika nyumbani kwa mjomba, mjomba alimpa dawa  za miti shamba, kijana yule baada ya kula alikuwa sawa.

Baadae mjomba pamoja na kijana yule walikaa katika mkeka kwa ajili ya kupata chakula. Chakula chenyewe ulikuwa ni ugali wa mhogo pamoja nyama ya swala.

Chakula kile kilikuwa ni kitamu sana kwani kilikuwa kimepikwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Wakati wanaendelea kula huku hadithi mbalimbali zilikuwa zimetawala mahali pale kwani muda mrefu ulikuwa umepita bila wao kuonana. Lakini katika ya maongezi yao mjomba hakusahau kumpongeza kijana yule kwa kuhitimu masomo yake ya chuo.

Basi huku maongezi yao yakiendelea walijikuta chakula kimeisha bila hata wao kujua. Hivyo kijana yule akaona asiwe mchoyo wa fadhira hivyo akaamua kumshukuru mjomba kwa chakula kitamu, lakini zaidi alisema ya kwamba alifurahishwa na nyama ile.

Lakini mjomba alimuahidi siku iliyofuata kwamba wangeambatana pamoja kwenda kuwinda pamoja. Kijana yule alifurahi maneno hayo kutoka kwa mjomba wake kwani alitamani kujua mbinu amabazo zilitumika kuwinda. Kwani alimini ule usemi "usimpe mtu samaki" bali mpe samaki siku ya kwana siku inayofuata mpe nyavu akavue mwenye.

Ilipofika asabuhi na mapema kila mmoja aliamka akiwa ni mzima wa afya tele, kijana alimuuliza mjomba wake ni muda gani ambao wangeenda mawindoni? Mjomba akamwambia ya kwamba muda wa kufanya mawindo ni muda wa usiku ambapo wanyama wengi huwa wamechoka sana. Hivyo ingefaa waendee muda usiku.

Hivyo ilipofika usiku mjomba pamoja na kijana yule walichukua dhana za uwindaji kwa ajili ya kuelekea mawindoni. Harakati za mawindo zilikuwa zimepamba moto katikati ya msitu, lakini matarajio yao yalikuwa hayapo sawa kwani hawakupata hata mnyama mmoja lakini hawakukata tamaa waliendelea kufanya mawindo.

Muda ulizidi kwenda bila ya kupata chochote. Kijana yule alikuwa amechoka sana, kwani aliamini ya kwamba kufanya mawindo ni kitu rahisi sana. Kwa kuwa kijana yule alikuwa amechoka sana, licha ya kuchoka alikuwa tayari ana usinginzi mzito, Hivyo mjomba aliamuru washushe hema ili waweze kupumzika. Waliingia ndani ya hema na kulala ndani ya hema.

Baada ya dakika chache wote walipitiwa na usingizi mzito ndani ya hema lile, baada ya masaa machache mjomba alishtuka usingizini hivyo akaamua amuamshe kijana yule. Mjambo alimuasha kijana yule, kijana aliamka, mjomba akamuuliza kijana "unaona nini angani?"  kijana akajibu naona nyota pamoja na mwezi unaoangaza kwa mwanga mzuri.

Mjomba akauliza tena "unachokiona kinamanisha nini? Kijana akajibu ya kwamba kile anachokiona ni ishara ya kwamba  Mungu yupo pamoja nao, pia mng'ao wa nyota zinaonyesha ya kwamba siku uliyofuata ilikuwa ni njema . mjomba akasema umejibu vyema, lakini tumeibiwa hema hivyo kikubwa zaidi nilitegemea utajibu ya kwamba "tumeibiwa hema" 

Mwisho umejifunza nini kupitia kisa hiki?

Tafsiri ya kisa hicho ni;

Kisa cha hadithi hii ni kwamba wapo baadhi ya watu wamekuwa na maisha magumu kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa  kupambanua vitu kwa mapana, hata hivyo naweza nikasema tumekuwa tukiishi katika hali ya kimazoea. Wengi tumekuwa tukitazama mambo kwa kuanza na vitu ambavyo vinaonekana mbali kuliko kuanza na vitu vilivyopo karibu.

Kwa mfano wahitimu wengi wa vyuo huamini ya kwamba baada ya kuhitimu masomo yao ni ajira, wao hawaamini ya kwamba wanaweza kujiri. Wapo baadhi ya watu ambao wanaishi mahali fulani wanawaza kwenda sehemu nyingine huku wakiamini kufanya hivyo ni njia ya mafanikio kwao, lakini ukweli ni kwamba kila mahali ambapo leo hii upo pana fursa.

Hivyo chunguza kwa umakini na uweze kujua  fursa zile ambazo zinakuzunguka ndipo uje kuwaza fursa ambazo zipo nje na hapo ulipo.

Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba kiporo hakihitaji moto mwingi, maana yangu ni kwamba mafanikio yako hayahitaji mambo makubwa sana ila yanahitaji kujiongeza zaidi kwa kila kitu ambacho unakifanya.

Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya,
0757909942

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.