Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, December 29, 2016

Hata Kama Huna Pesa, Ukiwa Na Kitu Hiki Kitakufanikisha.

No comments :
Inawezekana umekata tamaa kwa sababu unajiona mipango yako inaenda hovyo, huna pesa na hivyo unajiona huwezi kufanya kitu cha kukusaidia tena kufanikiwa kwa sababu ya hali hiyo uliyonayo.
Pengine usichokijua, kipo kitu kimoja ambacho huwa kinatoa mwelekeo na dalili ya mafanikio hata kama wakati huo huna pesa. Unapokuwa na kitu hicho ni rahisi kupiga hatua za kimafanikio. Kitu hiki si kingine bali ni matumaini.
Unapokuwa unaishi kwa matumaini ya kutambua kwamba utafanikiwa huku lakini ukichukua hatua karibu kila siku, ni rahisi kuweza kubadilika katika maisha yako na kuwa mtu wa mafanikio.
Inapotokea umeshindwa lakini ukawa una tumaini la kufanikiwa, hiyo itakupa nguvu tena ya kujaribu kitu kipya katika safari yako ya mafanikio uliyonayo.
Matumaini yanakupa nguvu ya kufanya zaidi na zaidi hata kama unachokifanya unaona kama hakilipi kwa sasa, kwa sababu una matumaini ya kufanikiwa, ni lazima utafanya hata kama upo kwenye hali ya mbaya kimafanikio.

Unaweza ukawa una maumivu makubwa ya kushindwa kwa kile unachokifanya na pengine umekata tamaa kabisa, lakini matumaini yatakuamsha na kusema fanya tena.
Lakini hata hivyo, ili uweze kuwa tumaini sahihi la mafanikio yako mara nyingi tumaini  haliji hivihivi, ipo gharama ambayo unatakiwa kuilipia ili kupata tumaini sahihi la kufanikiwa kwako.
Huwezi kukaa tu, halafu ukategemea upate tumaini au kitu cha kukupa faraja ni lazima ufanye kitu cha tofauti kila siku. Ni lazima uchukue hatua ya pale ulipo na kutaka kwenda sehemu nyingine.
Ikiwa utakuwa ni mtu wa kukaa tu na bila kuchukua hatua, elewa kabisa utahangaika sana na utakuwa mtu wa kukosa tumaini karibu kila siku ya maisha yako na kuiona dunia haifai.
Hakuna kisingizio chochote katika hili, tumaini la mafanikio yako ni matokeo ya wewe kuwajibika kwako kila siku. Ikiwa huwajibiki sahau kuwa na matumaini, utakuwa ni mtu wa kukatishwa tamaa kila siku.
Watafute watu ambao ni wakata tamaa maarufu, uangalie maisha yao yalivyo, utagundua ni watu ambao mara nyingi hawachukui hatua sahihi za kuweza kubadili maisha yao.
Kitu unachotakiwa kufanya ni kujenga tumaini jipya la mafanikio yako, kufanya kitu hata kama ni kidogo ambacho lakini unaamini kitabadilisha maisha yako.
Kwa kuishi maisha hayo hiyo itakusaidia sana kujitengenezea matumaini makubwa kwa maisha yako na utapata hamasa ya kufanya mambo mengi yakuweza kubadili maisha yako.
Kitu cha kukumbuka tumaini lolote lile linajengwa kwa wewe kuchukua hatua ya kufanya kitu fulani ambacho unaamini ni msaada kwako, vinginevyo itakuwa ni ngumu sana kufanikiwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


No comments :

Post a Comment