Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, December 1, 2016

Matumizi Sahihi Ya Muda Yanavyoweza Kukupa Mafanikio.

No comments :
Mwandishi mmoja wa kitabu cha "Mikasa ya Maisha" alieleza mengi sana  kuhusu maisha ambayo ameyapitia mpaka kufikia ndoto zake, lakini katika kitabu chake hicho nilijifinza mengi sana. Ngoja nichukue japo dakika chache kuweza kukushirikisha kwa kile ambacho nilijifinza katika kitabu hicho.

Mwanzano mwa kurasa za awali katika kitabu hicho alianza kwa kusema:
Kitendawili..............
Unaweze ukaitikia (Tega.......!)

Ni kitu gani kirefu kuliko vyote? Na pia wakati huohuo ni kifupi kuliko vyote?

Na kitu hicho hicho, wakati mwingine kikitumiwa vizuri huleta faraja, na endapo kitatumiwa vibaya huleta majuto. Mwandishi akauliza je, ni kitu gani hicho?


Je wewe mwenzangu unafikiri ndio ungekuwa katika chumba cha mtihani umeulizwa swali hilo ungejibu nini? Maana hata mimi wakati najiuliza juu ya kitendawili hicho nilikosa majibu, wakati nafikiria majibu, nikaona niendelee kwenda sambamba na mwandishi ili kujua kusudio la swali lake. Basi mwandishi akasema ya kwamba kitu hicho ni "MUDA"

Mwandishi akaendelea kusema ya kwamba muda ni kitu cha dhania tu, ambacho mtu huhisi, pia muda hauwezi kuishika kwa kutumia mikono. Akaendelea kusema ya kwamba muda umegawanyika katika sekunde, dakika, masaa, siku, wiki, mwezi, mwaka. 

Lakini pia muda kama huna jambo la kufanya huonekana ni mrefu sana, hapa ndipo tunapokutana na wale ambao husema ya kwamba siku ya leo ilikuwa ndefu sana.

Pia muda ukiutumia vizuri katika uzalishaji mali huonekana ni mfupi, hii ni kutoka na vile ambavyo umejipanga katika kuuthamini muda, katika suala zima la kuweza  kufanya vitu vya msingi. Swali la kujiuliza hapa muda ulionao ni mrefu au mfupi, kama ni mrefu unafikiri ni kwanini usinipe majibu?

Lakini vile vile muda kama ukitumia vizuri wakati huu, huleta faraja kubwa sana maishani. Watu wengi hushindwa kuutumia muda vizuri wakati bado wana nguvu na mwisho wa siku huja kulalamika mbeleni ya kwamba maisha ni magumu, yote hayo hutokea hasa pale mtu anaposhindwa kuitumie leo yake vizuri.

Hivyo ni vyema ukaitumia leo yako vizuri ili uweze kuitengeneza  kesho yenye furaha na faraja kwako.

Nimesema hayo kwa sababu watu wengi hufa na ndoto zao kwa sababu ya kutokutambua umuhimu wa muda, jambo hilo hutokea kwa sababu wao waliamini ya kwamba mafanikio yao yataanza kesho, lakini ukweli ni kwamba mafanikio huanza leo haijalishi utaanza kwa hatua ndogo kiasi gani.

Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio ni vile ambavyo utaamua kuutumia muda ambao uanao, hata uwe ni muda kidogo kiasi gani bali utumie kwa manufaa.

Ndimi; Mkeleketwa Wa Mafanikio Afisa mipango Benson Chonya

No comments :

Post a Comment