Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, December 6, 2016

Sahau Kuhusu Elimu, Mafanikio Yako Yanahitaji Kitu Hiki Kwanza.

No comments :
Moja kati ya uongo mkubwa, ambao umekuwa ukijidanganya na kufanya ushindwe kufanikiwa ni kule kuamini kwako kwamba, eti hujafanikiwa kwa sababu hujasoma sana au huna shahada toka chuo chochote.
Ili kupata matokeo unayoyahitaji katika maisha yako ikiwa pamoja na kufanikiwa haihitaji uwe umesoma sana, bali mafanikio ni matokeo ya kuweka nguvu na juhudi kwa kile unachokifanya kila siku.
Kama unaendelea kuamini hujafanikiwa kwa sababu hukusoma hili ni kosa kubwa sana unaloendelea kulifanya kwenye safari yako ya mafanikio na linakukwamisha pia.
Je. hivi unajua kwamba dunia imejaa watu wengi sana na waliofanya mambo makubwa bila kuwa na elimu kubwa kama ya chuo kikuu kama unavyofikiri?
Inawezekana hujui hili ndio maana unarudi nyuma kimafanikio kwa kuendelea kuamini uongo huo ambao unajirisha pole pole. Lakini ngoja nikwambie hivi tena, maisha yana washindi wengi sana ambao hawakusoma sana.
Biashara.
Richard Branson ambaye ni mfanyabiashara mkubwa dunia na mmiliki wa kampuni ya ‘virgin’ ambapo chini yake zipo kampuni ndogo ndogo 500, aliacha shule akiwa na umri wa miaka 15 na hakurudi tena.
Pamoja na kuacha shule katika umri huo, aliamua kutafuta mafanikio yake bila sababu. Leo hii mafanikio yake ni makubwa sana na inasemekana anao utajiri unaofikia kwa sasa dola za kimarekani bilioni 5.

Viwanda.
Katika eneo la viwanda tunaona Henry Ford hakuwa na elimu ya chuo kikuu. Elimu yake ilikuwa ni ya kawaida tu. Hata hivyo huyu ndiye moja ya wagunduzi wa kwanza wa gari na alifanikiwa kutengeneza kiwanda chake cha magari.
Wagunduzi.
Steve Jobs anatajwa kama ni mtu ambaye alikaa chuo miezi sita tu. Hilo halikumuzuia kutumia maarifa yake, matokeo yake aliibuka kuwa ni moja ya wagunduzi wakubwa duniani, yeye aligundua kompyuta aina ya ‘apple.’
Waandishi.
William Shakespeare aliacha shule pia na hakuweza kuendelea na masomo, lakini huyu ndiyo mwandishi aliyapata kugundua maneno zaidi ya 2000 ya lugha ya kiingereza na pia kuandika kazi zingine nyingi za kifasihi kwa lugha hiyo.
Sayansi.
Albert Einstein alishindwa kabisa mtihani ambao ulitakiwa umwezeshe kuingia chuo kikuu. Lakini Albert ni moja ya mtu ambaye alitokea kuwa na mchango mkubwa sana katika mambo ya sayansi katika karne ya 20 mpaka leo.
Muziki.
Hapa pia tunamwona mwanadada Aretha Franklin, hakuweza kuendelea na shule kwa sababu ya kupewa ujauzito akiwa na umri wa miaka 14. Hata hivyo alitumia kipaji chake cha uimbaji na kuibuka kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kuimba muziki aina ya ‘Rock’ .
Ukiangalia orodha hii ya watu waliofanikiwa bila kuwa na elimu kubwa ni ndefu mno na inaendelea tena na tena.
Watu hawa na wengine wengi ukiwafatilia utagundua kilichowafanikisha ni matokeo ya kuweka nguvu, juhudi na kuondoa hofu zote zinazowazuia kufanikiwa, hicho ndicho kilichotokea na ndio siri ya mafanikio yao.
Kumbuka wakati wote mafanikio sio elimu ya chuo kikuu peke yake, bali mafanikio ni matokeo ya kuweka nguvu na juhudi kubwa kwa kile unachokifanya kila siku.
Bila kuweka juhudi na nguvu kubwa, hata uwe na elimu kubwa vipi huwezi kufanikiwa na hilo liko wazi. Ni vyema ukatambua nguvu na juhudi yako ndiyo itakayokupa mafanikio haijalishi uwe umesoma au hujasoma.
Nikutakie kila la kheri katia kuelekea mafanikio makubwa.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment