Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, May 17, 2017

Jinsi Unavyoweza Kutengeneza Bahati Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Sina shaka umeshawahi kukutana na watu ambao wewe kwa haraka haraka ulikiri watu hao wana bahati sana katika maisha yao. Labda nikuulize tena je, umeshawahi kukutana na watu wenye bahati na hadi na wewe kutamani kuwa kama wao?
Hapa sitaki unipe jibu, baki nalo kimya kimya ila ninachotaka kukwambia ni kwamba hata wewe unaweza ukawa na bahati na ukawa na mafanikio. Naona unaanza kushangaa, sikiliza, yapo mambo mawili tu ya kukufanya ili uwe na bahati.
Kama utaweza kuyatumia mambo haya vizuri na kwa ufasaha basi jiandae na wewe kuitwa mtu wa bahati, ingawa bahati kama bahati kiuhalisia haipo kwenye maisha. Unashangaa? Ndiyo haipo, ila inatengenezwa, kivipi?  

Bahati inatengenezwa.
Kwanza, tafuta fursa ambapo pale wengine hawaoni.
Fursa yoyote unayoitafuta katika maisha yako haiji hivi hivi tu inakuja kwa wewe kuwa na jicho la kuona vitu vya ziada ambavyo wengine hawawezi kuviona. Kama una uwezo huo wa kuona yale ambayo wengin hawaoni, hapo ndipo wengine wataanza kuona  una bahati.
Utakua pale ambapo watu wengine labda wanalalamika maisha ni magumu lakini wewe pale ndipo unapoona kitu cha kufanya. Ili kufanikiwa na kuwa na jicho la namna hii ni lazima ujue kufikiri kwa utofati.
Anza kufikiri watu hawa wanapata chnagamoto gani kubwa, kipi kinachowasumbua? Ukishaligundua hilo wape watu hao kitu hicho na kila kitu kitaweza kufanikiwa na kuwa cha mafanikio makubwa na wengine watakuona ni kama vile una bahati.
Tatizo la watu wengi hawataki kufikirisha bongo zao. Wanataka kuwa ni watu wa kulala na kuamka bila kuwaza ni kipi cha kufanya au ni kipi ambacho jamii inakihitaji na wakitumie kama fursa ya kutoka kimaisha.
Karibu siku zote watu wenye jicho la tatu, watu ambao wanaona mapema fursa kuliko wengine hao ndio hujikuta wakiitwa ni watu wa bahati. Je, leo na wewe unataka kuwa mtu wa bahati, tafuta fursa ambapo pale wengine hawaoni.
Pili, jiandae kwa fursa.
Wale watu wanaoitwa watu wa bahati ni watu wa kujiandaa na fursa, ni watu wa kukaa na kuachia masikio yao huko na kule na kuangalia fursa sahihi kwao ambayo inaweza kuwafanikisha na kufika kwenye kilele cha mafanikio.
Kujiandaa kwa fursa hakuji hivihivi tu unatakiwa ujenge nidhamu. Na nidhamu inajengwa sana kwa wewe kuamua kuweka juhudi zaidi karibu kila siku ili uweze kufanikiwa kwa unachokihitaji  maishani mwako.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona unatakiwa ujenge nidhamu ya kujifunza, unatakiwa ujenge nidhamu ya kukusafanya mtaji na pia unatakiwa ujenge  nidhamu ya kuwa na matumizi mazuri ya pesa yatakayoweza kukupelekea ukawa mwekezaji mzuri.
Kwa kujua mambo hayo mawili yaani kutafuta fursa ambapo kuna wale wengine hawaoni na kujiandaa na fursa ni mambo ambayo yana uwezo wa kukufanya na wewe ukaonekana na wewe una bahati katika maisha yako.
Nikutakie siku njema na kila la kheri katika kufikia ndoto zako zikawa za kweli.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
dirayamanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment