google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 4, 2017

Mambo Matatu Yakuepuka Katika Safari Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Kuna wakati umekuwa unajilaumu kwamba maisha yamekuwa ni magumu, wengine husema wamelogwa, wengine husemwa hawana bahati na meneno mengine kama hayo.  Hizo sababu zinginezo ni woga binafsi ambao kimsingi kama utaendelea kuzibeba basi kufanikiwa kwako itakuwa ni ngumu. Lakini ukweli ni kwamba adui  namba moja wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Na adui huyu ni mbaya sana, kwani hatima ya maisha yako unayo mwenyewe, kwanini ubaki kuwanyoshea vidole watu wengine? Na ili hali wewe ndio mmliki mkuu wa maaumuzi yako? Nilichogundua ni kwamba watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu ya mambo haya;
1. Kusubiri mtu mwingine akufanyie maamuzi.
Kama tulivyosema hapo awali ya kwamba maisha  yako yapo mikononi mwako kwanini uache mtu mwingine afanye maamuzi juu ya maisha yako? Na jaribu kuwaza kwa sauti ila sipati majibu.Nasema hivyo kwa sababu maisha yetu yanakuwa ya kawaida kwa sababu tunapenda kuwaruhusu watu wengine watoe maaumuzi katika kutenda jambo fulani.
Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa jaribu kutafakari juu ya maisha yako na uamue kutoa maaumuzi juu ya jambo hilo. Lakini pia baada ya kutafakari ni nini cha kufanya jambo la msingi ni kuhakikisha unapata mtu sahihi wa kukushauri ni nini ufanye katika jambo hilo ili uwe bora zaidi.

Fanya maamuzi yako sahihi.
2. Kukata tamaa mapema.
Watu wengi sana huwa tunaathiriwa na ugonjwa huu wa ukataji tama mapema, na hii ni kwasababu wengi wengi wetu huwa tunapenda matokea ya papo kwa papo. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya papo kwa papo hakuna labda uamue kucheza bahati nasibu.
Ila kama unataka matokeo ya uhakika na yenye kuleta mafanikio ya kweli unachokihitaji ni kuwa mvumilivu kwa kila hatua ambayo unapiga kila siku katika jambo ambalo unalolifanya.
Hivyo niweke nukta katika maelezo haya kwa kusema ya kwamba kuwa mvumilivu kila wakati. Kwani mvumilivu hala mbivu, ila  kumbuka kuongeza hatua za kiutendeji ambazo zitakufanya uweze kusonga mbele na si kukata tamaa. Kwani kukata tamaa ni chukizo mbele za Mungu wetu.

Usikate tamaa mapema
3. Kuridhika mapema.
Kuridhika mapema ni adui mkubwa wa mafanikio yako, naomba hili libaki kichwani mwako. Mafanikio hayana ukomo, kila siku na kila wakati ona kabisa bado hujafanikiwa hata kama watu wanasema umefanikiwa. Usibweteke na hali uliyonayo. Daima kumbuka ya kwamba "Mafanikio ni njaa isiyoisha" hivyo kuridhika ni kurudi nyuma katika hali ya kiutendeji.
Nimalizie kwa kusema tena mafanikio hayana ukomo, hivyo achana na tabia ya kuridhika mapema.
Ndimi afisa mipango; Benson Chonya
0757909942

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.