Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, May 31, 2017

Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo.

No comments :
Hapo zamani za kale kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alijulikana kwa jina la mhavila. Mfalme huyu alikuwa na utu sana kwa watu wake. Japo kutokana na majukumu yake ya hapa na pale ilikuwa ni ngumu sana kwake kuonana na watu wake  mara kwa mara.
Kila mwakijiji wa jamii ile alitamani sana kukutana uso kwa uso na mfalme mhavila, kwa kukuwa mfalme huyu alikuwa ni mtu mcheshi sana kwa watu wake. Siku moja mfalme mhavila aliandaa mkutano mkubwa sana ambapo kila raia wa eneo lile alihudhuria katika mkutano ule.
Watoto kwa wakubwa, vijana kwa wazee wote walimiminika katika mkutano ule. Mfalme mhavila aliwaeleza watu wake mambo mbalimbali ambayo kimsingi yalikuwa yana manufaa sana katika kufanikisha masuala ya  maendeleo ya jamii na maendeleo ya watu hao kwa ujumla.
Mara baada ya mkutano kuisha mfalme mhavila alikutana na mtu mmoja ambaye alikuwa ni mjane, mjane huyo alionekana kwa macho ni maskini wa kutupwa, tunaweza kusema hivyo hii ni kutokana na muonekano wake. Mjane yule alimtazama mfalme mhavila kwa macho yenye kutia unyonge sana, baada ya dakika chache ndipo mjane yule akafungua kinywa chache na kusema;
‘’samahani mfalme mhavila kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta nafasi ya kuzungumza na wewe ila kwa bahati mbaya nafsi hiyo sikuweza kuipata, ila kwa siku ya leo nina kila sababu ya kumshukuru Mungu wangu kwa sababu tumeweza kukutana.
Kabla ya mfalme hajainua kinywa chache mjane akandelea kusema ‘ nafahamu ya kwamba upo bize na shughuli za hapa na pale, na unafanya hii yote kwa sababu ya kusongesha kurudumu hili la maendeleo, kwa kufanya hivyo nikupongeze sana kwa sababu kila mwenye macho na maskio anakiona na kukishuhudia kwa kile ambacho anakifanya.
Mfalme mhavila baada ya kusikia vile moyo wake ulikwenda kasi kidogo, hii yote ilikuwa ni mshangao wa kile ambacho mjane alichokuwa amemueleza, mfalme mhavila aliwaza kidogo, kisha akatafakari ndani ya nafsi yake. kisha mfalme mhavila akajibu asante sana mama kwa kutambua mchango wangu kwa kile nikifacho, kwa kweli nakushukuru sana.
Wakati watu wengine wakishangaa na kujihoji mama mjane na mfalme walikuwa wanazungunza nini, hakuna aliyepata majibu.
Hivyo mara ya sekunde chache mama mjane akamwambia mfalme mhavila ‘’ samahani mfalme mhavila nafahahamu ya kwamba una majukumu mengi sana, ila naomba jioni ya leo uje tule   kwa pamoja chakula cha jioni nyumbani kwangu.
Mara baada ya mama mjane kuzungumza hayo, mfalme mhavila akainua kinywa chake na kusema “ nashukuru sana mama kwa maneno yako yenye kunitia nguvu za kiutendaji wa kimaendeleo, kwani ulichokisema kimenipa fikra mpya za kuleta mbadiliko mapya ya kimaendeleo, hivyo nakuahidi siku ya leo tutajumuika kwa pamoja katika kupata hicho chakula cha jioni kwa pamoja.
Baada ya mazungumzo hayo mfalme mhavila na mama mjane waliagana na kuahidiana kukutana hiyo jioni kama ilivyopangwa. Mama mjane  alielekea nyumbani kwake kwa ajili ya kuandaa chakula hicho. Baada ya dakika chache chakula hicho kilikuwa kipo tayari, hivyo mama mjane akaweka chakula hicho mezani kwa ajili ya kuliwa. Mama mjane alimsubiri mfalme kwa muda wa saa nzima, lakini cha ajabu ni kwamba mfalme mhavila hakufika .
Mama mjane hakuchoka kumsubiri mfalme mhavila kwani alimini atakuja kama ambavyo walivyokuwa wapenga, muda ilizidi kwenda laikini mfalme hakuonekana kufika. Hivyo mama mjane akaamua kufunga mlango wake  kwa kuwa muda ulikuwa umeshakwenda.
Ilipita nusu saaa tangu mama mjane afunge mlango wake lakini cha ajabu mfalme mhavila hakutokea, wakati mama mjane anatafakari ni nini ambacho kitakuwa kimemsibu mfalme mhavila ghafla akasikia mlango ukigongwa. Mama mjane aliinuka mahali alipokuwa ameketi na kuelekea mlangoni kwa ajili ya kufungua.
Kabla mama mjane haujaufungua mlango , mama mjane alifurahi sana kwani aliaamini aliyekuwa amegonga mlango alikwa ni mfalme mhavila. Taratibu mama mjane akashika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kuufungua mlango. Mara baada ya kufungua alistajabu kumbe aliyekuuwa akigongo mlango hakuwa mfalme mhavila bali alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anatokwa na jasho sana. Hivyo yule kijana hakupoteza muda, alimsabahi mama mjane kisha kueleza shinda yake moja kwa moja. Kijana yule akasema samahani mama nimetoka mbali sana sehemu ambayo ni jangwani , hivyo nimetembea muda mrefu bila kunywa maji, hivyo naomba unisaidie niweze kupata maji ya kunywa.
Mama mjane alipatwa na hasira kidogo kwa sababu alitegemea ambaye aligonga mlango huenda alikuwa ni mfalme mhavila. Basi mama mjane alimtazama yule kijana kisha akelekea ndani na kuchua maji ambayo alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na kumpa yule kijana.
Mara baada ya yule kijana kunywa yale maji alimshukuru mama mjane, kisha kijana yule akaondoka. Mama mjane alirudi ndani kwa ajili ya kumsubiri mfalme. Lakini cha ajabu mfalme hukuweza kufika. Mama mjane alitafakari na kusema haiwezekani ni kwanini mfalme hakuweza kutimiza ahadi?
Wakati akitafakari hayo mara akasikia tena sauti ikitokea mlangoni, mama mjane alifurahi  sana kusikia sauti ile ikibisha hodi kwani nafasi hii aliamini yule aliyekuwa akibisha hodi alikuwa ni mfalme mhavila. Hivyo pasipo kupoteza muda mama mjane alielekea mlangoni kwa ajili ya kumfungulia mfalme mhavila.
Mara baada ya kufungua mlango ailikutana na mtoto mdogo ambaye mama mjane hakuweza kumfahamu mtoto yule, mama mjane alijaribu kuvuta taswira ni wapi ambapo aliwahi kumuona mtoto yule, mama mjane alikosa majibu kwani mtoto yule alikuwa ni mgeni machoni pake.
Mtoto alimsabahi mama mjane kisha akasema “ samahani mama yangu  nimetoka nyumbani kwetu wazazi wangu wameniacha tangu asubuhi, sijaweza kula chochote, hivyo naomba unisaidie chakula niweze kula mama yangu, kwani naumwa na njaa sana mama.
Mama alimtazama mtoto kwa macho yenye huruma sana, hivyo kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana aliamini ya kwamba mfalme mhavila hawezi kufika kwake tena, hivyo alichukua chakula  ambacho alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na kumpa mtoto yule. Mtoto yule alikula na kumshukuru mama mjane.
Mama mjane alifunga mlango tena na kuamini ya kwamba mfalme mhavila asingeweza kuja tena. Wakati akiwa ameketi ndani mwake mama mjane alisikia watu wakija uelekeo wa nyumba yake wakiimba nyimbo nzuri na za kupendeza sana. Alitafakari kuna nini? Wakati anazidi kutafakari sauti zile zilikuwa zinazidi kusogea katika nyumba yake.
Mama mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme mhavila akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini mfalme mhavila kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme mhavila alifika kwa mama mjane na  kusema asante sana kwa kunijali.
Mama mjane aliwaza na kusema mfalme mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati sijamfanya chochote?
Je mfalme Mhafavila alimshukuru mama mjane kwa kipi hasa? Usikose itaendelea wiki ijayo siku kama ya leo,
Ndimi afisa mipango Benson Chonya
0757909942

No comments :

Post a Comment