Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, May 27, 2017

Mambo Muhimu Ya Kufanya Ili Kuitawala Biashara Yako Kwa Mafanikio.

No comments :
Mafanikio katika biashara ni kitu ambacho karibu kila mafanyabishara anataka kitokee kwake. Wafanyabiashara na wajasiriamalia karibu wote, wana kiu na shauku kubwa ya kutaka kuona biashara zao zikifanikiwa.
Hata hivyo pamoja na kiu hiyo, lakini ukweli unabaki pale pale, kwamba suala la kutawala biashara na ikakupa mafanikio si jambo la kubahatisha bali yapo mambo ya muhimu ambayo wewe binafsi unatakiwa uyafanye ili biashara yako iweze kufanikiwa.
Bila kupoteza muda, fuatana nami katika makala haya ili nikuonyeshe mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyafanya katika biashara yako na kuifanya biashara hiyo ikawa ya mafanikio makubwa.
1. Kubali kuwa mwanafunzi wakati wote.
Tafuta maarifa kila siku ya kukusaidia katika biashara. Jifunze kuhusu washindi katika biashara zao ni kipi wanachokifanya na hata wale wanaoshindwa ni kwa nini pia wanashindwa. Kila unapojifunza hiyo inakupa nguvu ya kujiamini  na kufanikiwa. Kama ulikuwa hufanyi hivyo hebu anza sasa kujifunza zaidi juu ya biashara yako.

2. Chukua tahadhari kubwa kwenye biashara yako.
Ili biashara yako iweze kufanikiwa, unatakiwa kujua namna ya kuchukua tahadhari kubwa kwenye hiyo biashara. Unatakiwa kuchukua tahadhari ya nidhamu binafsi katika matumizi ya pesa na mambo mengi chungu nzima ya lazima ili kukuza biashara yako. Ikitokea ukakosa tahadhari hizo si rahisi sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara.
3. Unahitaji kutengeneza mtandao mzuri wa kibiashara.
Mara nyingi biashara inakuwa na kustawi vizuri sana hasa pale kunapokua na mtandao mzuri wa kibiashara. Hivyo ni vyema kujenga mtandao mzuri wa kibiashara na wafanya biashara wenzako, hali ambayo itakupelekea kuweza kukua kimafanikio katika biashara. Huhitaji kukaa kama kisiwa, jenga mtandao wa mafanikio ya biashara yako.
4. Unahitaji kuchukua tafahadhari ya afya yako.
Huwezi kufanikiwa kwenye biashara au katika maisha kwa ujumla kama afya yako ni mbovu. Unatakiwa kila wakati kuhakikisha afya yako inakuwa imara ili ikuwezeshe kufanya mambo mengi yakayoweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara kila wakati na kusiwe na kipangimizi.
Kumbuka haya ni mambo ya msingi sana ambayo unatikiwa uyazingatie kila wakati na kuyafanya  ii kuweza kuifanya biashara yako ikawa ya mafanikio makubwa. Chukua hatua na fanyia kazi mambo haya.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri katiika kufikia mafanikio yako makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0628 92 9816,

No comments :

Post a Comment