google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 2, 2017

Tumia Mbinu Hii Ili Kupata Majibu Ya Changamoto Inayokukabili.

No comments :
Je wewe ni miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika maisha? Kama jibu ni ndiyo makala hii inakuhusu sana, cha msingi nakusihi usome makala haya mwanzo hadi mwisho.
Maisha ya mwanadamu yamejawa na changamoto na shida mbalimbali. Changamoto hizo hizo, wapo baadhi ya watu huzivumilia katika kutenda jambo fulani, lakini pia wapo baadhi ya watu hukata tamaa kabisa. Na hao ambao hukata tamaa ndio ile idadi kubwa ya watu ambao hufa ni ndoto zao mapema.
Lakini ukweli ni kwamba changamoto na shinda mbalimbali za maisha ni kipimo cha akili, kwani wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo huimba katika nyimbo zao na kusema changamoto ni majaribu, na majribu ni mtaji. Hivyo katika maisha haya ni jambo la ajabu sana kama utaendelea kukataa tamaa katika maisha yako kwani hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa.
Na ukweli ni kwamba ili uweze kufanikiwa wanasema changamoto hazikwepeki, na changamoto ndio njia ambayo itakufikisha kule ambapo unataka kufika, endapo tu utaamua kupambana na changamoto hizo.
Swali linakuja nawezaje kupambana na changamoto hizo?
Jambo la msingi unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapambana na changamoto za maisha ni;
Orodhesha changamoto zote ambazo zinakukubali. Hata kama zipo zaidi ya changamoto tano ziandike zote.
Baada ya kuorodhesha changamoto hizo tano, jambo ambalo unatakiwa kufanya baada ya hapo unatakiwa kuchugua jambo ambalo lina umuhimu sana katika kulitekeleza.
Baada ya kulipata jambo hilo, usiishie kulichagua tu. Tafuta mbinu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo. Na mbinu hizo ziandikwe mahali ambapo panaonekana na uanze utekelezaji mara moja.
Mbinu hii ya kupambana na changamoto itakusaidia sana katika kupiga hatua mbele zaidi kivitendo kuliko kukata tamaa.
Nimekupa mbinu hii, kwa sababu wengi wengi huwa tunajitenga na changamoto za kimasha hasa pae zinapojitokeza.
Lakini kama nilivyoeleza hapo awali ni kwamba changamoto za kimaisha ni kigezo tosha cha kuweza kutimiza ndoto yako, jambo la msingi tafuta majibu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo.
Kama hutatafuta majibu ya changamoto zinazokukabli itakuwa ni sawa na bure, kwani utazidi kuwa maskini maisha yako yote.
Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya,
0757909942

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.