google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 15, 2015

Hii Ndiyo Nguvu Hatari Inayoaminiwa Na Wengi Katika Mafanikio.

No comments :
Vitendo vinavyohusisha masuala ya uchawi vimeenea sana ndani ya jamii yetu, na vimekuwa ndivyo gumzo kubwa sana miongoni mwa watu katika jamii. Na siyo hapa kwetu tu, bali hata katika nchi kubwa zilizoendelea nako ni hali kama ya hapa kwetu.

Kuna  baadhi ya watu ambao wanaona na kuhisi kwamba, uchawi ni ushirikina na mazingaombwe ambayo watu hawapaswi kuyatilia maanani. Kwa maoni ya watu hawa, uchawi ni mambo ya kidhahania tu. Hata hivyo, kwa walio wengi, uchawi ni jambo zito sana. 

Kulingana na watafiti wa masuala ya uchawi , wao wanasema kwamba, zaidi ya nusu ya watu ulimwenguni kwa namna moja ama nyingine wanaamini kwamba, uchawi ni kitu au nguvu halisi ambayo inaweza kuathiri au kudhuru maisha ya binadamu.

Mamilioni ya watu duniani wanaamini kuwa uchawi ni mbaya, hatari na unapaswa kuogopwa sana. Kwa mfano, sehemu kubwa ya nchi za Afrika, imani katika mizungu, ulozi na nguvu nyingine za aina hiyo imekolea sana katika maisha ya kila siku ya wakazi wa bara hili na hata kusababisha wachawi na walozi kuwa ni watu wanaochukiwa na kuogopwa sana katika jamii mbalimbali za kiafrika.

Lakini, labda suala la msingi tunalopaswa kujiuliza ni kwamba, kwa nini idadi ya watu wanaoshiriki na kukumbatia vitendo mbalimbali vya kichawi na kishirikina inazidi kuongezeka kwa kasi kubwa kila kuchapo? Na watu hao wako tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ili waweze kuhudumiwa na wachawi hao.


Mara nyingi kwa hapa kwetu sio ajabu kusikia mtu akisema kuwa, yuko tayari hata kuuza nyumba yake ya thamani pamoja na mali nyingine, ili apate fedha za kutosha kwenda kwa waganga kuulizia habari au kupiga ramli kwa lengo la kutaka kufahamu chanzo cha kifo au vifo vya watu wao wa karibu.

Watu wengi hivi sasa katika jamii yetu, kila wanapokwama kidogo katika masuala mbalimbali ya kimaisha, basi haraka huona ni bora kukimbilia kwa mafundi ili wakatafutiwe ufumbuzi wa shida zao.


Dhana hii ya uchawi na ushirikina kwa ujumla inajaribu kumuonesha na kumwelezea binadamu kuwa, ni kiumbe asiyejiamini na wakati wote huamini kwamba, kuna nguvu nyingine iliyo nje yenye uwezo mkubwa kuliko wake. Wakati wote hudhani kwamba, ni kupitia nguvu hiyo pekee iliyo nje yake, ndipo anapoweza kusuluhisha na kutatua migogoro yake ya kimaisha inayomkabili.

Kwa wakazi wengi wa Afrika na Asia, suala la uchawi au ushirikina kwa ujumla, kwao ni jambo la kawaida sawasawa na kufanya biashara ya njugu sokoni. Kwa hiyo kwa maneno mengine, hii ndiyo nguvu inayoaminiwa na wengi kuwapa mafanikio katika maisha yao.

Hata hivyo, baadhi ya sababu kuu zinazowafanya watu wavutiwe zaidi na uchawi au ushirikina ni kama ifuatavyo: wengi wao wanaona kuwa, uchawi unauwezo mkubwa wa kuwaondolea umaskini na mateso yanayoambatana  nao.

Pia wapo wanaoutumia katika suala zima la kufanikisha mapenzi, ikiwa ni pamoja na kuwavuta na kuwadhibiti wapenzi wao.

Wengine huamini uchawi unaweza matatizo ya kindoa, kizazi, kibiashara na kujiongezea bahati au kurekebisha nyota zao kwa kuondoa nuksi na mikosi. Kuna wengine ambao hutumia uchawi na ushirikina ili kupata kazi wanayoitamani, kupandishwa cheo makazini, kukuza na kufanikisha biashara zao, bila kusahau kutafuta utajiri. Na bado wengine huvutiwa na uchawi na ushirikina kwa sababu ya udadisi tu.


Jamii yetu hata hivyo, ina mifano mingi hai inayohusu suala zima la kukithiri kwa vitendo vya uchawi na ushirikina miongoni mwa watu. Hapa nitajaribu kueleza kwa uchache tu. Kwa mfano imani ya kudhaniwa mtu amekufa wakati yuko mahali amefichwa na mchawi, kuchukua mazao shambani kwa mwingine, kuua biashara ya mtu ama kumfanya mtu aondoke kwao na kutokurudi tena.

Hii ni baadhi tu kati ya mifano mingi ya nguvu ya kichawi kama zinavyoaminika katika jamii. Zamani, mambo ya kuamini uchawi yalikuwa yakifanyika kwa siri kubwa sana, lakini kwa sasa yako wazi. Siku hizi hata majirani wakigombana kidogo tu kuhusu mipaka ya maeneo yao  hawaishii kutishiana kuwa watalogana. Mwingine anaweza kusema kwamba, ‘ukileta mchezo nitakuendea kwetu kukushughulikia tuone kama baada ya mwezi mmoja hutaanza kuokota makopo’ na mambo mengine mengi.

Na mwisho ili mtu aweze kuondokana na kujiepusha na hofu ya uchawi na ushirikina, anapaswa kutupa na kuharibukila kitu kinachohusiana na uchawi, hii ni kama amejiingiza kwenye vitendo vya kichawi.

Pia, anapaswa kujenga imani thabiti kuelekea yale anayotaka kuyatimiza katika maisha yake. Imani hii isiyoyumba, itamsaidia sana kudhibiti uchawi kutoka kwa wengine au kujizuia asijiingize kwenye vitendo vya kishirikina.

Vilevile ni mtu kuamini kwamba, kuna nguvu nyingi, lakini ili nguvu ikuumize ni lazima uikaribie kwa kauli na vitendo vyako. Kama ukitenda na kutoa kauli muafaka, ni vigumu uchawi kukudhuru, kinyume cha hapo ni lazima kuwe na maumivu.

Tunakutakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio yako, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.