May 30, 2015
Haya Ndiyo Mambo Mawili Usipokuwa Nayo Makini Yatakutesa Na Kukusumbua Sana Katika Maisha Yako.
Hebu jaribu kufikiria iwapo unaona kwamba maisha yako hayakuendei vema, huku watu wengine unaofahamiana nao, pamoja na majirani zako, maisha yao yakiwaendea vizuri bila shida yoyote ile. Wenzako hao wananunua magari, wanajenga majumba, wanasomesha watoto wao katika shule nzuri na wanaishi maisha mazuri kuliko wewe. Je wewe utawazaje? Utajisikiaje? Utawaonea kijicho ama?
Ni kweli kabisa kwamba, kuna
wakati ambapo huwa tunataka kuwa na kila kitu, ili kuoekana kuwa na maisha bora
pengine hata zaidi ya hao wengine tunaowaona. Lakini swali la msingi hapa
tunalopaswa kujiuliza ni kwamba, je, katika hali halisi jambo hili
linawezekana?
Kulingana na maoni ya Jo Anne White ambaye ni profesa wa elimu
katika chuo kikuu cha Temple nchini
marekani, ni kwamba kijicho huonesha ile hali ya mtu kujitazama na kujijali
yeye mwenyewe. Ni suala linalohusu namna watu wanavyojihisi kujielekea wao
wenyewe na iwapo kweli wanajiamini kuhusu namna walivyo.
Kijicho na wivi ni kama
ndugu mapacha. Kwa mfano, unaweza kuona wivu iwapo mwenzi wako wa ndoa
hakujali. Vilevile wivu unaweza ukachochewa endapo mwenzako wa karibu atakufanya
usijisikie vizuri kwa kutumia maneno ya kuumiza na vitendo pia.
Ikumbukwe pia katika
uhusiano wowote ule, kuaminia, kutamaniana na kuheshimiana kwa dhati ni mambo
muhimu katika kufanya uhusiano huo ustawi na kuimarisha mawasiliano yenye
nguvu.
Vilevile kama mtu ana picha
mbaya na isiyo na nguvu kujihusu, mara nyingi anaweza kuhisi kutishiwa na
kuamini kwamba, hana lolote atakaloweza kuchangia katika kumfanya mtu yeyote yule
avutiwe naye.
Kwa kawaida, mwanzoni tabia
ya wivu inaweza ikaonekana kuwa ni hali fulani ya urafiki, hasa iwapo mtu wako
wa karibu atahitaji muda wako mwingi wa kumjali na inaweza pia kuwa ni dalili
ya kukosa ukaribu kwenye hisia.
Ni ukweli ulio wazi kwamba,
suala la wivu huweza kuibuka pale mtu anapohisi kukosa usalama na kutishiwa,
ama kwa kuhofia kupoteza uhusiano wake au kwamba mtu mwingine badala yake
anathaminiwa kama yeye ambvyo alikuwa akithaminiwa.
Hata hivyo wivu hauko kwenye
uhusiano wa kimapenzi tu, pia upo kwenye mafanikio ndio kitu ninachotaka
kuzungumzia hapa kama nilivyoanza makala hii. Kwani, mtu ambaye hana picha
kubwa na yenye kujielekea yeye mwenyewe atakuwa ni rahisi kwake kuhisi kwamba
watu wengine wanamuonea wivu na kijicho kwa mafanikio yake.
Kulingana na maoni ya Debbie
ambaye ni mwandishi wa kitabu kiitwacho Turn
off your inner light: Fitness of of body, mind and soul, ni kwamba, wanaume
wengi hupatwa na hali ya kijicho kinachohusiana na kujipatia mali, kama vile
kazi nzuri, heshima au hadhi fulani,nyumba nzuri, ambapo kwa upande mwingine,
wanawake wao huwa ni mwenye kijicho kuhusiana na mwonekano wao ikiwemo sura,
watoto na marafiki zao.
Ili kuweza kukabiliana na
kijicho katika maisha yetu, mtu anapaswa kutambua uwezo na nguvu zake, kwa
maana kwamba anamudu kufanikisha nini, nini malengo yake aliyojiwekea katika
maisha yake. Usijilinganishe na mtu au watu wengine, kwa sababu kwa kufanya
hivyo ni sawasawa na kuhujumu uwezo wako pekee.
Wahakikishie watu wengine na wewe mwenyewe kwamba, leo ni
siku yako na zamu yako kufanikiwa, na siyo kesho ila fanya hivyo kwa vitendo. Tumia
kijicho hicho hicho ulichonacho na kukuchochea uweze kukamilika na kukua. Hapa
tunasema kuwa na kijicho cha maendeleo. Jiambie, kuwa kama fulani ameweza , ni
wazi kwamba, inawezekana hata kwangu na nitafanya hivyo.
Kama kuna mtu ambaye
anapenyeza sumu ili kufanya uone wivu au kijicho katika jambo fulani, basi
unalazimika kubadili mada kwenye mazungumzo yenu au kama ni lazima jiondoe
machoni pa mtu huyo. Acha kuwa na kijicho ama wivu sana unaokuumiza wa
mafanikio yaw engine. Jipange na tafuta mafanikio yako, vinginevyo hayo ndiyo
mambo mawili usipokuwa nayo makini yatakutesa na kukusumbua sana katika maisha
yako.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza
zaidi kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.