Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, September 19, 2016

Aina Hii Ya Uhuru Ndiyo Itakayofanya Uwe Na Mafanikio.

No comments :
Ukimchukua ndege pori yeyote yule aliyezoea kuishi mwituni na kuamua kumpeleka katika eneo ambalo unaloishi kwa lengo la kumfuga, ndege huyo hata ukimpa kila kitu ataona unamtesa tu.

Unajua ni kwanini itaonekana hivyo ni kwa sababu ndege huyo anahitaji uhuru wa kihisia ambao hufanya kila mara awapo mwituni. Uhuru huo wa kihisia humfanya ndege awe huru zaidi na kufanya ndege huyu afanye vitu anavyovipenda zaidi kuliko kulazimishwa.

Katika maisha yeyote ya mwanadamu ili aweze kufanya jambo bora zaidi, anahitaji uhuru wa kihisia zaidi. Aina hii ya uhuru wewe ndiye ambaye unatakiwa kuwa mwenye maamuzi zaidi katika kutenda jambo fulani pasipo kuvunja sheria.

Watu wengi tunaishi maisha ambayo hayana  tija mara zote kwa sababu tumeshaozea kila kitu ambacho unakifanya unataka mtu fulani akwambie ufanye jambo hilo lakini kufanya hivyo ni kosa kubwa sana.

Tafuta uhuru wa kihisia, utafanikiwa.
Lakini kumbuka ya kwamba kwa jambo lolote unalolifanya katika dunia hii linahitaji kutendwa kwa uhuru zaidi, na kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo katika eneo husika ili liweze kutendeka kwa uhuru zaidi.

Leo hii biashara nyingi hufa kwa sababu mtu anayefanya biashara hiyo amekosa uhuru wa kihisia kwa maana anashindwa kutumia muda uliopo katika kufanikisha shughuli zake za kibiashara katika kutengeneza faida.

Hata pindi zinapojitokeza changamoto za kihisia humfanya aanze kuhususisha changamoto hizo na imani za kishirikina. 

Tazama kwa makini juu ya ndoa nyingi zilizipo katika kizazi hiki cha karne ya 21 jinsi zinavyovunjika, ndoa nyingi hufa kwa sababu ya kukosea kwa uhuru wa kihisia katika wanandoa hao.

Ndoa nyingi hakuna maandalizi ya kutosha katika kumfahamu mwenza wako, kuhusiana vitu ambavyo anavipenda na vile asivyopenda, katika masuala ya ndoa unahitaji kumfahamu mwenza wako kuliko kumjua tu.

Tumia muda mwingi katika kumfahamu mwenza wako hii itakusaidia kuweza kushirikiana ninyi kama wana ndoa katika kujua masuala ya uhuru wa kihisia ambao utasababisha upendo wenu uweze kukua mara dufu zaidi.

Tuangazie macho japo kwa ufupi mambo ya msingi katika kutengeza uhuru Wa kihisia;

1. Siku zote kuwa na ratiba yako binafsi ambayo itakuongoza kuweza kutenda mambo ya msingi pasipo kumtegemea mtu aweze kukupangia mambo ya kufanya.

2. Fanya mambo yaliyo chanya zaidi, kufanya hivi kutakusaidia kuweza kuishi kwa amani na upendo na kuweza kutengeneza amani ya moyo.

3. Tambua kuwa maisha yako anayejua ni wewe, hivyo nidhamu katika matumizi ya muda ni ya kwako.

4. Mwisho tambua ya kwamba maisha yako ya leo ni matokeo ya kile ulichokifanya jana, hivyo ni vyema ukaiandaa leo yako vizuri ili uweze kuishi kesho yako yenye baraka na Mafanikio tele.

Ni vyema ukapata uhuru wa kihisia leo, maana kutakufanya uweze kutenda vitu kwa kupenda, kwani ukifanya vitu kwa kupenda kutoka nafsini mwako hata matokeo yake huwa chanya pia.

Kama unapenda kujifunza zaidi juu ya maisha ya mafanikio, karibu kwenye group la WHATS APP ili ujifunze zaidi sheria na mbinu mbinu mbalimbali za mafanikio.
Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, ikifuatiwa na jina lako kwenda 0713 04 80 35, hapo utaunganishwa bure na kuianza safari yako ya mafanikio kwa USHINDI ZAIDI.
Karibu sana na tupo pamoja.
Ndimi, Afisa mipango Benson Chonya.

No comments :

Post a Comment